Katika Kijiji cha Shaviringa ndogo ya makuchi kaunti ndogo ya Hamisi, Kenya, mvulana wa miaka 13 amejitoa uhai kwa kujinyonga na kamba
Chifu wa kata ya Shiru, Josephine Khalwale amesema kuwa mvulana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano kabla ya kujiua alichukua kitu kwenye kibanda cha jirani yao na mmiliki alipomshtaki kwa wazazi aliadhibiwa na baada ya hapo alitoweka
Wazazi wake walianza kumtafuta jioni na waliupata mwili wa mtoto wao saa 4 usiku ukiwa umening'inia kwenye nyumba moja isiyo na wakazi ndani yake
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya rufaa ya Vihiga