Mwanafunzi wa kike DSM ajinyonga kupinga kusoma

Mwanafunzi wa kike DSM ajinyonga kupinga kusoma

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Bertha(1).jpg


Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Tegeta jijini Dar es Salaam, Bertha Amir (14),amejinyonga hadi kufa akipinga kulazimishwa na mama yake mzazi kusoma.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya SekondariTegeta jijini Dar es Salaam, BerthaAmir (14), pichani, amejinyonga hadi kufa akipinga kulazimishwa na mama yake mzazi kusoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema mwanafunzi huyo alijinyonga juzi saa 11:00 jioni, maeneo ya Tegeta Namanga, jijiniDar es Salaam.

Alisema marehemu alikutwa amejinyonga chumbani kwa kutumia mtandio ulioninginizwajuu ya dari.

Kamanda Wambura alisema sababu za mwanafunzi huyo kujinyonga bado hazijafahamika, lakini akasema inasadikika kuwa wakati wa enzi za uhai wake, siku moja kabla ya kifo chake, alikuwa ameongea na mama yake, Angelina Maiko Mshami (30), ambaye alimtaka achukue fedha kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule.

Alisema mtoto huyo alimjibu mama yake kuwa hahitaji kusoma, bali anataka kufanya kazi.

Kamanda alisema kuwa mwili wamwanafunzi huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi na kwamba, polisi wanaendelea na upelelezi kuhusiana na kifo chake.

Akizungumza na NIPASHE nyumbani Tegeta jana jioni, mama wa mtoto huyo, Angelina Mshami, alisema alishangazwa nakitendo cha mtoto wake kuamuakukataa shule ghafla wakati alikuwa ana uwezo mzuri darasani.

Alisema kuwa mtoto wake alikuwa na akili darasani akishikanafasi ya kwanza ama ya pili wakati akisoma shule ya msingi na hivyo kumfanya afaulu kujiunga kidato cha kwanza.

Hata hivyo, alisema kabla ya kifo chake, binti yake alimweleza kuwa hataki shule bali anataka kufanya kazi.

Alisema alipomuuliza kazi gani anataka kuifanya, hakuitaja bali alisisitiza kuwa anaifahamu mwenyewe.

Betha ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wawili katika familia yao, alizaliwa mwaka 1999, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Malindi mkoani Tanga na kufanikiwa kujiunga na Shule ya Sekondari Mtumbi na baadaye kuhamishiwa katika Shule ya Sekondari Tegeta.

Aidha, baadhi ya majirani waliokuwapo msibani hapo, walielezea masikitiko yao na huzuni kuhusiana na kifo cha msichana huyo.

Marehemu anatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea mkoani Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho kijijini Malindi.


CHANZO: NIPASHE
 
Hapo itakuwa kuna jamaa lilikuwa linamdanganya kuwa aache shule amuoe amtafutie kazi afanye.
 
nafikiri kuna mkono wa mtu hapoa alikuwa hapendi huyo mtoto aendelee mbele
 
Binti mdogo Malala Yousafzai alipigwa risasi na Taleban akiwa darasani katika kile kilichoelezwa kama kuwazuia watoto wa kike kusoma. Malala hakuiogopa shule wala vitisho!,binti zetu mambo ni tofauti!
 
Kazi ya shetani hii...nina wasiwasi huyo binti alikuwa possessed!
 
Back
Top Bottom