Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Msichana wa miaka 17 (jina limehifadhiwa), aliyekatishwa masomo akiwa darasa la sita na kuozeshwa, amenusurika kifo baada ya kupigwa kikatili kwa madai ya kuchelewa kushika mimba. Tukio hili la kusikitisha linadaiwa kufanywa na mume wake, likitokea wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Mwanafunzi huyo kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, baada ya kuokolewa na wasamaria wema kwa kushirikiana na Shirika la Memute linalopambana na ukatili wa kijinsia.
Soma Pia: Polisi Lindi wadaiwa kumlinda askari anayeshukiwa kumbaka binti wa miaka 13
Inasemekana tukio hilo lilitokea Novemba 19, 2024, ambapo msichana huyo alifungwa kwenye mti kabla ya kushambuliwa vibaya, hali iliyomwacha na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Hadi sasa, watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ili kufanikisha kumkamata mtuhumiwa mkuu wa tukio hili la kinyama.
Source: Wasafi FM