Mwanahabari auawa na wasiojulikana Cameroon

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mtangazaji na Mwandishi maarufu wa Habari za Michezo nchini Cameroon Anye Nde Nsoh, ameuawa katika mji wa Bamenda uliopo Kaskazini Magharibi mwa nchi.

Ripoti zinasema kuwa Nsoh alikuwa kwenye baa alipovamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kwa risasi.

Kwa miaka mingi sasa Bamenda imekuwa moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi na migogoro iliyopo kati ya wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza waliojitenga.

Nsoh alikuwa mtangazaji wa Dream FM Radio ya Bamenda na Mwandishi wa habari za michezo katika majukwaa mbalimbali mitandaoni.

Waandishi wengine wawili wa Cameroon waliuawa katika miezi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Younde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…