TANZIA Mwanahabari, Prudence Karugendo afariki Dunia

Hakika Mola ndiye alitoa, na pia ndiye aliyemtwaa mja wake Prudence Karugendo. JINA lake Mola na lizidi kuhimidiwa. Amina.
 
Mkuu, tumeshafanya maombi - usiwe na wasi - hakuna lisilowezekana kwa Bwana wa Majeshi
 
Serikali ijitokeze wazi iseme nin kinatokea kwa vifo vya ghafla namna hii na wanaokufa wanadalili za corona, kwann watu wasiseme ni corona hata kama sio korona.
Kwenye hii habari, wametaja dalili zozote?
 
Hakika,tusoropoke tuu!
 

Marehemu Prudence Karugendo wakati wa uhai wake

BARUA YA WAZI KWA JPM: KAIBANJA WALIA NA UMEME
(Makala ya Mwisho ya Mwandishi Prudence Karugendo Tarehe 24/12/2020)


Na Prudence Karugendo

Kaibanja ni moja ya kata zinazotengeneza halmashauri ya Bukoba Vijijini katika wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera. Kata hiyo iko umbali wa kilometa 50 kutoka kwenye mji wa Bukoba ambako ndiko makao makuu ya mkoa wa Kagera yaliko. Huo ni umbali ambao ni mfupi sana ambapo katika baadhi ya sehemu zenye miji mikubwa kama vile Dar es salaam bado wananchi wa Kaibanja nao wangeitwa wakazi wa mjini.

Lakini kutokana na kuwa katika sehemu ya vijijini eneo la kata ya Kaibanja linaonekana kusahaulika sana sawa na maeneo mengi ya mashambani, kitu kinachowafanya wakazi wa eneo hilo wajione sio tu kwamba wametengwa na jiografia bali pia wametengwa na wahusika wanaoshughulikia miundombinu ya nchi.

Mfano mmowapo ni huduma ya umeme; pamoja na kwamba kwa kipindi kirefu sasa kuna mradi wa kitaifa wa umeme vijiji, REA, ambao umewaboreshea mambo mengi wananchi wa vijijini, bado wananchi wa Kaibanja walio wengi wanaishia kuziona nyaya tu za umeme huku wakiuona umeme huo ukiwaka katika vijiji vingine vya mbali na kwao!

Lakini wenyewe wakibaki gizani bila kunufaika na nishati hiyo kwa namna yoyote!
Hilo ni jambo lililomhuzunisha sana Sheikh Mohammad Abdallah, mkazi wa kata Kaibanja lakini akiishi na kufanya kazi ya kiroho katika kata ya Ibwera, na kuamua kutafuta ufumbuzi wa suala hilo kupitia gazeti la JAMHURI.

JAMHURI lilipotembelea maeneo ya Kaibanja limekutana na mwenyekiti wa kijiji Kaibanja, Emmanuel Bagandanshwa, ambaye ameweza kuelezea kwa kirefu adha wanayoipata wananchi wa Kaibanja kuhusu umeme. Mwenyekiti huyo anasema ni zaidi ya miaka 10 tangu itangazwe kuwa watapatiwa umeme, lakini waliishia kuona tu mashamba yao yakifyekwa kuwa inatafutwa njia ya umeme ambapo ilisimikwa milingoti isiyofikia 10 ambayo haikuunganishwa na nyaya za umeme na kisha nguzo hizo kuondolewa karibu zote na kuhamishiwa kwingine kusikojulikana! JAMHURI limeshuhudia nguzo zisizofikia 10 tu zilizobaki zikiashiria kuwa kuna mradi wa umeme kijijini hapo!

Wakati hali ikionekana hivyo wananchi wanaeleza walivyofyekewa mashamba ya migomba pamoja na mibuni kwa madai ya kupisha njia ya umeme lakini ikaonekana kwamba umeme huo umelengwa kwa watu maarufu tu bila wananchi wa kawaida kuhusishwa pamoja na wananchi hao kuharibiwa mashamba yao!

Umeme umepitishwa maeneo ya Kaibanja na kupelekwa vijiji jirani kama Kaishente ukiwatafuta watu maarufu tu! Ambapo vitongoji vya Ibanja na Kikunyu waliharibiwa mazao yao kupisha laini ya umeme waliyodhani inakwenda kwao lakini umeme ukawekwa sehemu moja tu inayoitwa Kakoronto ambayo ni senta ya sehemu hiyo!

Wananchi hao wa Kaibanja wanashangaa jinsi umeme ulivyokwepeshwa kwao na kupelekwa vijiji vya mbali kupitia porini kana kwamba wao hawana mahitaji nao wakati wao wako kwenye barabara kuu inayotoka mjini kuelekea sehemu moja maarufu, Katoro, na baadaye Kyaka katika wilaya ya Misenyi!

Ni kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kuonekana ni kikwazo cha kutowasha umeme katika eneo la Kaibanja kwa vile upo umeme uliowashwa kama majaribio ambapo nyumba kama 10 tu ndizo ziliwekewa umeme katika senta ya Kaibanja, anasema mwenyekiti wa kitongoji Kaibanja, Aliyu Abdallah.

Hiyo tu inaonesha kwamba umeme unaweza kuwaka katika kata ya Kaibanja bila matatizo yoyote. Ila hiyo tu haiwezi kuwa faraja tosha kwa wakazi wa Kaibanja sababu bado kuna maeneo ambayo yanahitaji umeme kama yalivyo mahitaji ya umeme kote unakopatikana.

Mfano zipo taasisi nyeti ambazo umeme ni muhimu na wa lazima kama vile makanisani na misikitini, madrasa na shule za awali zahanati nakadhalika, ambavyo vinahitaji kuwa na nishati hiyo ambayo kukosekana kwake kwenye maeneo hayo nyeti kunawafanya wakazi wa Kaibanja kuonekana wakiwa!

Mara nyingi imesemwa kwamba wananchi hawapaswi kujiona wakiwa yanapokuja masuala muhimu kwa jamii kama umeme na maji, ni haki na halali yao. Kwahiyo wananchi wa Kaibanja hawategemei kuona mtu anayefanya kitendo cha kuweka umeme kwenye kata yao kionekane kama hisani!

Wananchi hao wanaipongeza serikali kwa mpango wake wa REA, umeme vijijini, ila wanajiuliza kwa nini watumishi wachache wa serikali, kwa maana ya watumishi wa TANESCO, na wengine wenye mamlaka wafanye “mazabe” kitu kinachoonekana kama kuichonganisha serikali na wananchi kwa kufanya mambo tofauti na watumishi hao wanavyoelekezwa? Kwa nini watumishi wa aina hiyo waendelee kuvumiliwa wakati watu wanaohitaji kazi kama wanazozifanya wao wako tele!

Ikumbukwe rais amesema kwamba asingependelea wananchi wamsimamishe njiani kila mara kumweleza kero ambazo tayari yeye kaishateua na kuajiri watu wa kuzitatua.

Serikali inafanya mipango ya kuwaondolea kero wananchi lakini ikiwatumia watumishi wanaoshindwa kuwajibika, bora ikawaondoa na kuwatafuta wengine wanaoweza kukizi haja.

Kuwavumilia watumishi wazembe ni kujiletea migogoro isiyo ya lazima, ni kuwafanya wananchi waichukie serikali yao bila sababu ya msingi. Ni heri kuwapiga chini watumishi hao ili wananchi wapate huduma zinazotolewa na serikali yao kwa muda na mpangilio muafaka!,

Mfano, Mzee Hamza Mohammed Kasinde wa kitongoji Kaibanja, anasema haitoshi umeme kuuona tu kwenye senta yao, tuseme Kaibanja mjini, anatamani ufike hata kwake na kwa majirani zake. Anasema yeye ni mgonjwa wa taarifa za habari lakini vyombo kama redio na luninga anashindwa kuvitumia kwa kukosa umeme!

Watumishi wa umma wapo kuwaboreshea wananchi maisha yao kutokana na mikakati iliyowekwa na serikali yao, wale wanaoikwaza ili kuwafanya wananchi waichukie serikali yao ni bora kuwapukutisha wakabaki au kuwekwa wale walio tayari kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Bwana Charles Kahatano Lwempisi ni mwekezaji ambaye kaishajenga kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo, majengo na mashine viko tayari, lakini anashindwa kuanzisha uzalishaji kutokana na tatizo la kukosa umeme! Kaishalipia kila kitu kinachotakiwa na shirika la umeme, TANESCO, ila haoni umeme!

Pia Bwana Lwempisi kajaribu kuitikia wito wa Rais Magufuli wa kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za wageni ila ukosefu wa nishati bado unaufanya uwekezaji huo liwe jambo lisilotabilika!Richard Rugalabamu ni mtu mwenye makazi Dar es salaam na Mwanza, lakini asili yake ni Kaibanja.

Kama ilivyo kawaida ya Wahaya, kajenga nyumba nzuri sana kijijini kwake tatizo nyumba hiyo haina umeme! Anategemea umeme wa jua, solar, na jenereta tu kuhudumia nyumba yake hiyo!

Kaibanja wameliona hilo, sasa ni zamu ya serikali kuliangalia kwa mtazamo mwingine kusudi wananchi hao wakipate kile wanachokihitaji ambacho ni huduma ya umeme.

prudencekarugendo@yahoo.com
0654 031 701

Chanzo: Bukoba Wadau
 
Siku hizi hata mtu akifariki kwa nasibu kwenye ajali barabarani, basi ni korona!??? JPM kazi anayo kwelikweli. Nashauri Sisiemu iendelee kutawala tuuu hadi Tanzania [emoji1241] iwe zaidi ya Ulaya.
Nakuona kwenye ubora wako na JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…