Elections 2010 Mwanahalisi: CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa

Naanza kupata wasiwasi mkubwa zaidi! Kwa asilia ya mataifa ya kiafrika, pale wanapozidiwa nguvu na upinzani, hujeukia mapinduzi (sio mapinduzi kama yalivyoasisiwa na Mwl Nyerere)- CHADEMA mlindeni huyu mzee, watamtoa roho! Yaani huwezi ukaelewa- kwa nini isiwe ni kupokezana na madaraka, ni nini kinachowafanya CCM waone kama akipata huyu basi ni mwisho wao!

Nina imani kubwa kama CCM ingekuwa walau kwa kipindi kimoja chama cha upinzani, Tanzania ingenyooka sana. CCM ni dume inapokuwa upinzani, CHADEMA ingewabidi tu wafanye kila jema na kwa mstari ili tu wasiondolewe madarakani kabla ya muda wao. Hii inaleta hali murua katika uongozi bora. Kwa sasa hivi tulikuwa na upinzani mzege mzege(sijui ndio kiswahili).
 
Njilembera,
Mbona sababu ni rahisi sana? CCM wanaogopa wakiondolewa mamlakani wengi wao wataishia lupango. Madudu waliyoyafanya ni mengi sana kuanzia enzi za Mzee Ruksa, fisadi Mkapa na sasa msanii huyo. Watatafuta kila njia kuzuia mabadiliko ya kweli yasitokee.
 

Penye red: Fedha? Siyo fedha zitokazo mifukoni mwao, ni fedha zetu wenyewe wanazotuibia.
 
Waungwana wanamapinduzi mliopo huko nyumbani nawaomba mjaribu kuscan na kutuwekea habari kama hizi.Baadhi yetu tunaweza kuzitumia huku tulipo JUST IN CASE....
 

Mhhh....Hili halitatokea Tanzania, no matter who become President. Sana sana watatakiwa kurudisha mali walizoiba iwapo itathibitika mahakamani. Hatuna viongozi wenye hulka ya aina hii katika duru hili la siasa!!
 
Hii inaitwa Media politics hata Obama aliitumia, Chadema inaungwa mkono na magazeti hayazidi matatu lakini yanavyozichanga karata zake hutadhani upande mwingine unaungwa mkono na lukuki ya magazeti.
 
Ni wazi kwamba CCM watajaribu kutumia technicalities kumzuia Dr Slaa. Wanajua fika hawawezi kumshinda kwa hoja. Yeye ana hoja kubwa ya kupiga vita ufisadi. CCM wakisema watapiga vita ufisadi hakuna mtu atawaamini. Wameulelea miaka yote hii.

Hofu yangu ni kwamba CCM itatumia vibaya mahakama kumzuia Slaa. In vibaraka sehemu mbalimbali. Kitu kitakachotuepusha na mbinu chafu ni kujitokeza kwa Watanzania wengi kumuunga mkono Dr. Slaa. CCM haitataka vurugu. Slaa akiwa na wafuasi wengi mbinu chafu zitaogopwa.
 

Na ofcourse there is a bigger problem more than that, ok say Slaa amezuiwa CCM kampeni zao watafanyia wapi? Hii inaweza kuwa chanzo cha vurugu kubwa kama ilivyowahi kutokea nchi nyingine za Africa. Na kwa sababu for years sera za CCM zimekuwa zikizalisha the group with the name " We have nothing to loose" Shughuli yake lazima itakuwa pevu.
 

Hiyo red hapo juu: zoezi ili ni la kijinga na bila kufikiri na linanipa faraja kwani wadhamini hao 'feki' wamo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura; sasa ni makosa ya nani kama si National Electoral Commission (NEC)? Na ni kigezo kizuri sana cha mdhamini kuwa mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari la wapiga kura! Chadema hili likitokea basi uchaguzi usimamishwe kwa amri ya mahakama pamoja na gharama zote za maandalizi ili kutoa muda kwa NEC kushirikiana na uhamiaji kuhakiki daftari la wapiga kura. Pili CCM ndio wanafuga majitu sio raia ndani ya nchi yetu na ndio maana wimbi la ujambazi ni kubwa.

Kama ujinga huu utafanikiwa, nafikiri it is a hight time now to use our forests and streets to fight for our freedom!!
 
Hizo ndizo siasa lakini kwa watu makini hakuna wa kumzuia Dr. Slaa kugombea. nafikiri kwa vyama vingine vifurahi ili at least mwaka huu tupate upinzani kidogo kwa wale wanaotaka ushindi wa kishindo. Inabidi watu waache demokrasia ifanye kazi yake.
 
Watu wakijani kwa mawazo mafupi bado tu mnasubiri mkono udondoke, wenzenu leo wameanza kampeni nyie bado mnamawazo ya kizamani ya ushindi mezani, nendeni mkafanye kampeni si kusubiri mwingine awekewe pingamizi. NEC imeshawapitisha wagombea na wameshaanza rasmi kampeni kama hamjui hilo basi endeleeni kuota.
 
Hii move yao itashindwa tu. Kwa nini wanaogopa changamoto za kisiasa? You cowards!! mkia m a t a k o n i kama mbwa koko!!
Kheeee heeee heeee! si mbali, kumjua mbwa koko ni nani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…