Mwanajeshi kudhulumu darubini

Mwanajeshi kudhulumu darubini

Pelly

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
197
Reaction score
207
Habari za wakati huu,

Mimi ni mwananchi wa kawaida, raia wa Tanzania. Nipo Dar es Salaam katika eneo fulani ambalo lilikuwa shamba la marehemu mzee wangu, sasa limekuwa eneo la makazi. Ilibidi mzee apime viwanja na kuanza kuuza baadhi ya viwanja. Kuna mteja mmoja, mwanajeshi, alijenga na kuhamia yeye na mkewe, bado hawana hata mtoto. Iliyotokea, tukawa kama marafiki japo tabia tulikuwa hatuendani.

Kuna siku nilimuazima mtu darubini. Basi siku moja jioni nikasema ngoja nitoke nayo niangalie mazingira ya mbali. Kumbe alikuwa amekuja kwangu wamekaa chini ya mti. Alipoiona tu akachanganyikiwa, akanyanyua mkono eti harooh, "Umeipata wapi wewe? Siyo askari?" Nikamjibu, "Aliyekuambia hizi ni za askari tu nani?"

Wakati nafikiria kumpa, akatokea mke wa jirani yake ambaye walishagombana. Akaniita maana nafuga kuku, nikaenda kumkamatia kuku nimuuzie mida ya kumi na moja jioni hiyo. Nikamkabidhi, basi wakati nimesimama na shemeji tunaongea, mjeda akapita na darubini yangu kuelekea kwake, akasema nakuja sasa. Nikaendelea na mambo mengine, sasa nikawa nasahau kumuuliza. Iliyotokea baada ya kama wiki mbili, nikamuuliza, "Mbona hurudishi darubini yangu?" Akajifanya kushtuka, "Sijakuletea?" Nikamwambia, "Wacha ujinga." Akaanza kujizima data, eti kama nilileta siku fulani ile alikuja dada yako. Nikamwambia, "Siku ile nilikuona unatoka kwako hujabeba kitu na ulisalimiwa tukaongea kidogo nikiwa kwenye banda la kuku." Akajifanya, "Ooh, mbona siioni ndani basi nitaitafuta, mara basi nitalipa niambie sh ngapi nikulipe." Nikamkazia, "Hapana, naomba mzigo wa watu kwanza." Basi toka siku hiyo kanikazia eti alishanipa darubini. Sasa mimi naona sheria ifuate mkondo wake maana kamwaga ugali nami wacha nimwage mboga, sababu ananidharilisha kwa watu na sasa ni maadui tayari.

Naombeni nifuate hatua zipi ili kukomesha hii tabia. Kwanza amedhalilisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Naombeni njia zipi nifuate ili nimuone bosi wake tu. Ili ni jeshi letu sote jamani haki zitendeke.

Asanteni.
 
Ulizia kambi anayofanya kazi ukaripoti tangu siku hiyo atakuheshimu sana
Sina hakika japo anazungumziaga kambi 2 tofauti, nafikiri itabidi nitenge siku nikamuulizie huko kote tu
 
Hii nchi ni ya kipumbavu sana
Nilishawahi kushuhudia polisi wameenda kusachi nyumba ya mtu kwa kupewa taarifa kuwa mwenye nyumba ana darubini
Hii nchi imejaa kundi kubwa la wajinga
 
Ulizia kambi anayofanya kazi ukaripoti tangu siku hiyo atakuheshimu
Sahihi! Na uwaambie kabisa umeamua kuanza kwao,kablla hujapanda ngazi za juu...huyo mpuuzi atarudisha chap, na atakuogopa.
 
Habari za wakati huu,

Mimi ni mwananchi wa kawaida, raia wa Tanzania. Nipo Dar es Salaam katika eneo fulani ambalo lilikuwa shamba la marehemu mzee wangu, sasa limekuwa eneo la makazi. Ilibidi mzee apime viwanja na kuanza kuuza baadhi ya viwanja. Kuna mteja mmoja, mwanajeshi, alijenga na kuhamia yeye na mkewe, bado hawana hata mtoto. Iliyotokea, tukawa kama marafiki japo tabia tulikuwa hatuendani.

Kuna siku nilimuazima mtu darubini. Basi siku moja jioni nikasema ngoja nitoke nayo niangalie mazingira ya mbali. Kumbe alikuwa amekuja kwangu wamekaa chini ya mti. Alipoiona tu akachanganyikiwa, akanyanyua mkono eti harooh, "Umeipata wapi wewe? Siyo askari?" Nikamjibu, "Aliyekuambia hizi ni za askari tu nani?"

Wakati nafikiria kumpa, akatokea mke wa jirani yake ambaye walishagombana. Akaniita maana nafuga kuku, nikaenda kumkamatia kuku nimuuzie mida ya kumi na moja jioni hiyo. Nikamkabidhi, basi wakati nimesimama na shemeji tunaongea, mjeda akapita na darubini yangu kuelekea kwake, akasema nakuja sasa. Nikaendelea na mambo mengine, sasa nikawa nasahau kumuuliza. Iliyotokea baada ya kama wiki mbili, nikamuuliza, "Mbona hurudishi darubini yangu?" Akajifanya kushtuka, "Sijakuletea?" Nikamwambia, "Wacha ujinga." Akaanza kujizima data, eti kama nilileta siku fulani ile alikuja dada yako. Nikamwambia, "Siku ile nilikuona unatoka kwako hujabeba kitu na ulisalimiwa tukaongea kidogo nikiwa kwenye banda la kuku." Akajifanya, "Ooh, mbona siioni ndani basi nitaitafuta, mara basi nitalipa niambie sh ngapi nikulipe." Nikamkazia, "Hapana, naomba mzigo wa watu kwanza." Basi toka siku hiyo kanikazia eti alishanipa darubini. Sasa mimi naona sheria ifuate mkondo wake maana kamwaga ugali nami wacha nimwage mboga, sababu ananidharilisha kwa watu na sasa ni maadui tayari.

Naombeni nifuate hatua zipi ili kukomesha hii tabia. Kwanza amedhalilisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Naombeni njia zipi nifuate ili nimuone bosi wake tu. Ili ni jeshi letu sote jamani haki zitendeke.

Asanteni.
Huyu nadhani anafikiri kuwa unaitumia kumuwinda mkewe.
 
Jambo dogo nenda kambini katoe taarifa utapata msaada
 
Back
Top Bottom