ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Wakuu poleni na kazi.mimi sina kazi wala sina majukumu.mimi toka nije dar es salaam kwa ndugu yangu nikafikia maeneo ya chanika sikuwahi kupata nafasi ya kuzurura mjini.sasa leo asubuhi ndugu yangu kanipa nauli nikatembee tembee.sasa hivi nazurura mitaa ya posta kwenye maghorofa.jamani mjini pazuri sana Kuna maghorofa marefu mengine ya vioo.dar Kuna joto ninatoka jasho balaa.nitafika mpaka baharini nikapande ile meli niende kigamboni alafu narudi nayo Tena posta.na print mpaka k koo. Kwa hiyo jamani yoyote anayetaka kunifaham hii ndo nafasi yake.tukutane sehemu tuonane tubadilishane mawazo.nimebaki na 14000 kwa hiyo tutakula lanchi pamoja asiwaze kabisa.ni kwa hisani ya upendo tu.hata hivyo jf party together nitakuwepo nitashiriki SI shillingi 30000 TU nitaipata tu