MwanaKJJ Jumatano: Jaji Kaijage Anapata Shida Kusimamia Uchaguzi TZ?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
nec.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Nilivyoandika jana kuna watu wanaona sikusema kwa ukali sana. Wapo wanaosema naogopa kumnyoshea kidole Rais Magufuli kwa sababu nilimuunga mkono kugombea kwake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. Inachonishangaza ni kuwa hata watu wanaojua uandishi wangu wanafikiria kwa sababu fulani sijajiunga kwenye jukwaa la wanaotaka watafute uhalali wao wa kisiasa kwa kuonesha wanampinga Magufuli. Hili sina tatizo nalo na ndio maana ya uhuru wa fikra na maoni.

Hata hivyo, hatari ambayo ipo sasa kwa wanaharakati, wanasiasa, wanasiasa watarajiwa na watu wengine ni kuamua kufumba macho na kuwa wakali zaidi kwa kukosoa vitu na watu sahihi na kuwataka wawajibike. Rais Magufuli anabeba lawama zote za yale mambo ambayo yeye ndio mwamuzi wa mwisho na ambayo yanaweza kutatuliwa ama kwa ushauri wake au kwa maagizo yake rasmi (executive orders).

Kwa sasa, naamini kabisa siasa zetu zinaweza kubadilika kabisa, zikawa zakiungwana, zisizo na ulazima wa kumwaga damu na zisizojenga uhasama endapo vyombo hivi viwili chini ya viongozi wao wawili vitang’ang’aniwa na kulazimisshwa vifanye kazi yao inavyopaswa.

Hapa nazungumzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi la Tanzania. Hili ni wazi kwa watu wengi lakini labda uzito wake ndio wengi bado hatujaupata inavyopaswa na badala yake tunakimbilia kumdai Rais. Wapo watu wengi sana ukiwasoma pamoja na ujuzi wao wote na hata uzoefu wao wote, wanaonekana hawaamini kabisa wanapaswa kuving’ang’ania vyombo hivi viwili.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaundwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 74 na utendaji wake kazi unaongozwa na sheria na kanuni mbalimbali husika. Ni kweli kwamba, Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi huteuliwa na Rais; lakini hili si jambo geni. Nchi nyingi tu duniani tena za kidemokrasia zina mfumo ambapo Rais au Waziri Mkuu anateua wajumbe wa Tume za Uchaguzi. Suala kubwa kwa tume za uchaguzi si nani hasa anayeteua bali zaidi ni jinsi gani ziko huru kutoka kwa yule anayewateua.

Ni kweli kabisa, kwa mfumo wetu ulivyo, Tume ya Uchaguzi inamtegemea sana Rais. Hili hata hivyo, halimaanishi haiko huru kufanya kazi zake. Tatizo kubwa kwenye tume yetu ya Uchaguzi ni kukosekana kwa weledi (unprofessionalism) na hivyo kufanya kazi kinyume na kifungu cha 11 cha Ibara hiyo ya 74. Kiongozi yeyote wa tume (Mwenyekiti, Mjumbe au maafisa wa uchaguzi) wanaposikiliza, wanapofuata maagizo ya viongozi wa serikali au ya chama fulani cha kisiasa kama CCM kinyume na matakwa ya sheria na miongozo yao wanavunja Katiba.

Yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mdogo wa Kinondoni; chombo pekee kinachopaswa kubeba lawama zote za mapungufu yote yaliyotokea pale ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hii si mara ya kwanza kwa tume hii kuonekana inashindwa kuendesha uchaguzi kwa amani; na inaonekana kuzidiwa na misukumo na mihemuko ya kisiasa. Watendaji wake wanashinikizo kubwa la kusimamia haki na wakati mwingine inaonekana wanafanya kazi kwa woga au hofu fulani. Wapo waliojifunza kwa wenzao ambao waliwahi kuonekana kuadhibiwa au wengine kuzawadiwa.

Inawezekana vipi, tume miaka zaidi ya ishirini sasa ya kuendesha chaguzi mbalimbali bado inapata shida kuweka utaratibu mzuri kwa mawakala, wanasiasa, na hata kusimamia uchaguzi bila watu kuonekana wameonewa? Hivi ni kweli wote humo ndani ya tume hakuna mtu mwenye weledi na usomi wa kujaribu kutabiri (expect) matatizo mbalimbali yanayoweza kutokea kama jambo moja au la pili likitokea. Hivi ni kweli, tume haijaona jinsi gani masuala ya mawakala yanavyosumbua.

Hivi kwanini mawakala wa vyama vya siasa wanasubiri hadi siku moja kabla ya uchaguzi ndio wapate kukubaliwa? Kuna ubaya gani, kwa watu wenye akili timamu kusema tutengeneze utaratibu utakaohakikisha kuwa wiki moja kabla ya uchaguzi wowote – uwe mdogo au mkuu – kila chama kiwe kimeshapata kila kinachohitajika kuhakikisha kuwa mawakala n.k wanajulikana na wamepata utambulisho wote? Kwanini tusubiri hadi dakika za mwisho kama siyo kutengeneza mazingira ya watu kuonekaan wameonewa na kulazimisha watu wengine wajaribu kuweka shinikizo lisilo la lazima?

Leo hii tunawalaumu upinzani kwa kuandamana kudai mambo ya mawakala wao? Tuliwataka wafanye nini? Wakinge mikono na kuomba kama zawadi? Wote tumeona jinsi gani serikali na vyombo vyake vilivyotumiwa kwenye chaguzi hizi hasa Kinondoni; kweli kabisa tunataka Mahakama ndio ije baadaye kutengua uchaguzi huu huu halafu watu warudie tena kama vichaa wasiojifunza lolote? Binafsi naamini CHADEMA itakuwa na msingi mzuri tu wa kwenda mahakamani kupinga kuchaguliwa kwa Mtulia na sitoshangaa wakashinda! Lakini kwanini tufike huko?

Tatizo la utendaji wa Tume ya Uchaguzi ni kubwa mno, linatia aibu na linatufanya tujihoji kama tunaweza kuendesha uchaguzi sisi wenyewe bila kulazimisha uhasama, vurugu, na hisia za kuonewa. Niliuliza juzi; hivi kweli ni vigumu sana kwa Watanzania kuendeshsa uchaguzi kwa amani, kwa utulivu, na katika mazingira ya ushindani na siyo uadui? Kwanini tuendessha uchaguzi kama wale wengine wanaogombea wanatoka sayari ya Zebaki au Zuhura na hivyo hawastahili kabisa kuaminiwa au kupewa nafasi? Ni ukiritimba gani huu tulio nao kwenye fikra za kiutawala?

Hivi, kwa mfano CHADEMA wangeshinda Kinondoni katika mazingira ya uhuru, haki na usawa; hivi Kinondoni ingegeuka jangwa? Au wana CCM wa Kinondoni wangegeuka misukule? Si huyo huyoaliyegombea CCM alikuwa CUF na alishinda 2015 na Kinondoni watu waliendelea kuishi, kufanya shughuli zao na maisha yaliendelea? Au tu ni dalili kuwa inawezekana ipo haja ya kuanza kuandika tena na kusimuliza vile visa vya Ujinga wa Mwafrika? Kweli kabisa, tunashindwa kuendesha uchaguzi sisi kwa wasomi wetu, na watendaji wetu ambao waliapa kuendesha uchaguzi kwa haki na bila upendeleo wakizingatia Katiba?

Nani aliyesema kuwa tunahitaji amani zaidi siku ya kutumbukiza makaratasi kwenye masanduku kuliko mchakato mzima wakufikia siku hiyo. Kama uchaguzi ungekuwa ni kutumbukiza karatasi tu; sisi kampeni zinawekwa za nini? si lengo ni kushawishi watu kwa hoja. Sasa kama watu hawawezi kushawishi kwa hoja na badala yake wanatawaliwa na vihoja; kwanini isiamuliwe tu hakuna tena kampeni kama kampeni zinaudhi sana baadhi ya watu?

Matatizo yaliyomshinda Jaji Lubuva tunaona leo yanajirudia na kuwa ni magumu kushughulikiwa na Jaji Kaijage. Ina maana hawa majaji wanaweza kuwa ni mahiri wa sheria, lakini inawezekana ni viongozi wabovu. Kwanini mambo ambayo yanawezekana kama mtu akiwa thabiti yaonekane kuwa magumu hivyo? Kama wanaona hawawezi kufanya kazi bila kuingiliwa au mashinikizo mengine si waamue kujiuzulu kuliko kujiabisha kwa kuendesha mfumo ambao unadharaulisha kabisa dhana nzima ya haki, usawa, na ushindani wa kisiasa? Yaani, kama marefarii wa mpira wa miguu wangekuwa wanapata shida kama hizi; kweli kuna mechi ingekuwa inachezwa? Kama refarii angesikiliza mashabiki na wamiliki wa timu, kweli wangeweza kuchezesha mchezo wowote?

Tatizo la pili; ni Jeshi la Polisi. Sijasema tatizo ni Askari Polisi. Nimesema Jeshi la Polisi. Suluhisho langu kuhusiana na hili hapo kesho, likipokelewa na wenye kupokea na wakalifanyia kazi nawahakikishia kwa asilimia 90 litabadili kabisa mahusiano kati ya Jeshi na vyama vya upinzani na litatengeneza mazingira mapya kabisa ya kisiasa.

Itaendelea Kesho
 
Naona usingizi umeanza kukutoka, Hata hivyo mimi wala simlaumu Jaji Kaijage.. Tatizo pale ni yule Kada anayeitwa Kailima na kapewa madaraka makubwa sana pengine hata kumzidi Mkuu wa tume, ukimsikia akiongea ni kama vile anajiona yeye ndiye Mungu au massiah ajaye, Wanatuharibia nchi kwa sababu ya kuweka makada kwenye sehemu nyeti!
 
Hata Mimi sijapingana na Wewe, kumbe ulisoma comment yangu Mzee mwenzangu!! Ila nikuhakikishie hakuna mtu anayetaka au anayekulazimisha kuwa kwenye kambi yetu, usijipe moyo kwa hilo, halipo, kwenye vita askari mmoja akifa, akidondoka, akirudi nyuma kamwe hakuna haja ya kumlaumu, mnasomnga mbele. Kama ataona vyema basi atajiunga nanyi huko mbeleni (Nadhani ndio unachojaribu kukifanya sasa).

Back to the topic, nakubaliana na wewe kabisa; kuna muingiliano mkubwa sana kwenye hivi vitengo. walio wengi wako hapo kwa maslahi binafsi, hakuna anayetaka kupoteza kibarua chake. Ni aibu aibu aibu. Kuna siku tutaamka asubuhi tusiikiute Tanzania.
 
Hivi waliojiandikisha kupiga kura walikuwa wangapi, na waliopiga kura walikuwa wangapi? Je tunaolalamika tulikuwa miongoni mwa wapiga kura?
 
Kuna watu wanasema ati kwa vile Rais kasema kauli zake basi watumishi wanaondoa ufahamu kabisa. Ilitarajiwa baada ya Rais kusema alichosema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipaswa kutoa maagizo ya kuwataka watendaji wote kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sharia na Katiba na bila upendeleo. Angewataka wahakikishe aliyeshinda kwa halali ndio anatangazwa.

Tumezoea kulea tabia za uzembe na watu kutozingatia maadili yao ya kazi ndio maana tunazitolea udhuru. Mtu amepewa majukumu na anajua majukumu yake halafu anasema "anaingiliwa". Hivi huko wanakojifunza, hawajifunza kujiuzulu? Ina maana Tanzania watumishi wote hawana ujasiri wa kusema "mimi hili sifanyi"? Au ndio watu wanasema "njaa" kwa hiyo njaa imewaondoa kabisa weledi?

Ukikubali hili; unafikiri itakuwaje?
 
Nchi hii tulipofika, total destruction is the only solution. Tuanze alif kwa kijiti.
 
Naona mleta mada unazunguka mbuyu tu.
Tatizo kuu ni Magufuli. Narudia tena, tatizo kuu ni Magufuli. Jeshi la Polisi na Tume ya uchaguzi wanafanya huo upuuzi na uhuni wao hadharani kwa ujasiri na kujiamini kwa sababu wanajua wazi kabisa Magufuli yupo nyuma yao. Ndio aliyewatuma na ndiyye anayewalinda.

Chunguza mwenendo na matamshi Magufuli kuhusu mwenendo mzima kuhusu siasa, upinzani, uchaguzi na vyombo vya dola na hapo utapata jibu kamili.

Kama Tume ya uchaguzi inaweza kufanya ushenzi wote ule, na bado Magufuli anakuja hadharani kupongeza washindi bandia na kuipongeza tume ya uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi ule 'vizuri', hapo unategemea nini?

Kama jeshi la Polisi linaweza kuua binti mwanafunzi hadharani na Magufuli anakuja hadharani kuwapongeza kwa kazi nzuri ya usalama, hapo nategemea nini?

Badala ya kuwafukuza kazi viongozi wote wa juu wa wizara ya mambo ya ndani na jeshi la polisi, Magufuli yuko busy kuizinisha ahadi ya milioni 80 ili kugharamia mazishi ya binti aliyeuwawa na polisi ili kuzima mjadala.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nilivyoandika jana kuna watu wanaona sikusema kwa ukali sana. Wapo wanaosema naogopa kumnyoshea kidole Rais Magufuli kwa sababu nilimuunga mkono kugombea kwake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. Inachonishangaza ni kuwa hata watu wanaojua uandishi wangu wanafikiria kwa sababu fulani sijajiunga kwenye jukwaa la wanaotaka watafute uhalali wao wa kisiasa kwa kuonesha wanampinga Magufuli. Hili sina tatizo nalo na ndio maana ya uhuru wa fikra na maoni.

Hata hivyo, hatari ambayo ipo sasa kwa wanaharakati, wanasiasa, wanasiasa watarajiwa na watu wengine ni kuamua kufumba macho na kuwa wakali zaidi kwa kukosoa vitu na watu sahihi na kuwataka wawajibike. Rais Magufuli anabeba lawama zote za yale mambo ambayo yeye ndio mwamuzi wa mwisho na ambayo yanaweza kutatuliwa ama kwa ushauri wake au kwa maagizo yake rasmi (executive orders).

Kwa sasa, naamini kabisa siasa zetu zinaweza kubadilika kabisa, zikawa zakiungwana, zisizo na ulazima wa kumwaga damu na zisizojenga uhasama endapo vyombo hivi viwili chini ya viongozi wao wawili vitang’ang’aniwa na kulazimisshwa vifanye kazi yao inavyopaswa.

Hapa nazungumzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi la Tanzania. Hili ni wazi kwa watu wengi lakini labda uzito wake ndio wengi bado hatujaupata inavyopaswa na badala yake tunakimbilia kumdai Rais. Wapo watu wengi sana ukiwasoma pamoja na ujuzi wao wote na hata uzoefu wao wote, wanaonekana hawaamini kabisa wanapaswa kuving’ang’ania vyombo hivi viwili.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaundwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 74 na utendaji wake kazi unaongozwa na sheria na kanuni mbalimbali husika. Ni kweli kwamba, Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi huteuliwa na Rais; lakini hili si jambo geni. Nchi nyingi tu duniani tena za kidemokrasia zina mfumo ambapo Rais au Waziri Mkuu anateua wajumbe wa Tume za Uchaguzi. Suala kubwa kwa tume za uchaguzi si nani hasa anayeteua bali zaidi ni jinsi gani ziko huru kutoka kwa yule anayewateua.

Ni kweli kabisa, kwa mfumo wetu ulivyo, Tume ya Uchaguzi inamtegemea sana Rais. Hili hata hivyo, halimaanishi haiko huru kufanya kazi zake. Tatizo kubwa kwenye tume yetu ya Uchaguzi ni kukosekana kwa weledi (unprofessionalism) na hivyo kufanya kazi kinyume na kifungu cha 11 cha Ibara hiyo ya 74. Kiongozi yeyote wa tume (Mwenyekiti, Mjumbe au maafisa wa uchaguzi) wanaposikiliza, wanapofuata maagizo ya viongozi wa serikali au ya chama fulani cha kisiasa kama CCM kinyume na matakwa ya sheria na miongozo yao wanavunja Katiba.

Yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mdogo wa Kinondoni; chombo pekee kinachopaswa kubeba lawama zote za mapungufu yote yaliyotokea pale ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hii si mara ya kwanza kwa tume hii kuonekana inashindwa kuendesha uchaguzi kwa amani; na inaonekana kuzidiwa na misukumo na mihemuko ya kisiasa. Watendaji wake wanashinikizo kubwa la kusimamia haki na wakati mwingine inaonekana wanafanya kazi kwa woga au hofu fulani. Wapo waliojifunza kwa wenzao ambao waliwahi kuonekana kuadhibiwa au wengine kuzawadiwa.

Inawezekana vipi, tume miaka zaidi ya ishirini sasa ya kuendesha chaguzi mbalimbali bado inapata shida kuweka utaratibu mzuri kwa mawakala, wanasiasa, na hata kusimamia uchaguzi bila watu kuonekana wameonewa? Hivi ni kweli wote humo ndani ya tume hakuna mtu mwenye weledi na usomi wa kujaribu kutabiri (expect) matatizo mbalimbali yanayoweza kutokea kama jambo moja au la pili likitokea. Hivi ni kweli, tume haijaona jinsi gani masuala ya mawakala yanavyosumbua.

Hivi kwanini mawakala wa vyama vya siasa wanasubiri hadi siku moja kabla ya uchaguzi ndio wapate kukubaliwa? Kuna ubaya gani, kwa watu wenye akili timamu kusema tutengeneze utaratibu utakaohakikisha kuwa wiki moja kabla ya uchaguzi wowote – uwe mdogo au mkuu – kila chama kiwe kimeshapata kila kinachohitajika kuhakikisha kuwa mawakala n.k wanajulikana na wamepata utambulisho wote? Kwanini tusubiri hadi dakika za mwisho kama siyo kutengeneza mazingira ya watu kuonekaan wameonewa na kulazimisha watu wengine wajaribu kuweka shinikizo lisilo la lazima?

Leo hii tunawalaumu upinzani kwa kuandamana kudai mambo ya mawakala wao? Tuliwataka wafanye nini? Wakinge mikono na kuomba kama zawadi? Wote tumeona jinsi gani serikali na vyombo vyake vilivyotumiwa kwenye chaguzi hizi hasa Kinondoni; kweli kabisa tunataka Mahakama ndio ije baadaye kutengua uchaguzi huu huu halafu watu warudie tena kama vichaa wasiojifunza lolote? Binafsi naamini CHADEMA itakuwa na msingi mzuri tu wa kwenda mahakamani kupinga kuchaguliwa kwa Mtulia na sitoshangaa wakashinda! Lakini kwanini tufike huko?

Tatizo la utendaji wa Tume ya Uchaguzi ni kubwa mno, linatia aibu na linatufanya tujihoji kama tunaweza kuendesha uchaguzi sisi wenyewe bila kulazimisha uhasama, vurugu, na hisia za kuonewa. Niliuliza juzi; hivi kweli ni vigumu sana kwa Watanzania kuendeshsa uchaguzi kwa amani, kwa utulivu, na katika mazingira ya ushindani na siyo uadui? Kwanini tuendessha uchaguzi kama wale wengine wanaogombea wanatoka sayari ya Zebaki au Zuhura na hivyo hawastahili kabisa kuaminiwa au kupewa nafasi? Ni ukiritimba gani huu tulio nao kwenye fikra za kiutawala?

Hivi, kwa mfano CHADEMA wangeshinda Kinondoni katika mazingira ya uhuru, haki na usawa; hivi Kinondoni ingegeuka jangwa? Au wana CCM wa Kinondoni wangegeuka misukule? Si huyo huyoaliyegombea CCM alikuwa CUF na alishinda 2015 na Kinondoni watu waliendelea kuishi, kufanya shughuli zao na maisha yaliendelea? Au tu ni dalili kuwa inawezekana ipo haja ya kuanza kuandika tena na kusimuliza vile visa vya Ujinga wa Mwafrika? Kweli kabisa, tunashindwa kuendesha uchaguzi sisi kwa wasomi wetu, na watendaji wetu ambao waliapa kuendesha uchaguzi kwa haki na bila upendeleo wakizingatia Katiba?

Nani aliyesema kuwa tunahitaji amani zaidi siku ya kutumbukiza makaratasi kwenye masanduku kuliko mchakato mzima wakufikia siku hiyo. Kama uchaguzi ungekuwa ni kutumbukiza karatasi tu; sisi kampeni zinawekwa za nini? si lengo ni kushawishi watu kwa hoja. Sasa kama watu hawawezi kushawishi kwa hoja na badala yake wanatawaliwa na vihoja; kwanini isiamuliwe tu hakuna tena kampeni kama kampeni zinaudhi sana baadhi ya watu?

Matatizo yaliyomshinda Jaji Lubuva tunaona leo yanajirudia na kuwa ni magumu kushughulikiwa na Jaji Kaijage. Ina maana hawa majaji wanaweza kuwa ni mahiri wa sheria, lakini inawezekana ni viongozi wabovu. Kwanini mambo ambayo yanawezekana kama mtu akiwa thabiti yaonekane kuwa magumu hivyo? Kama wanaona hawawezi kufanya kazi bila kuingiliwa au mashinikizo mengine si waamue kujiuzulu kuliko kujiabisha kwa kuendesha mfumo ambao unadharaulisha kabisa dhana nzima ya haki, usawa, na ushindani wa kisiasa? Yaani, kama marefarii wa mpira wa miguu wangekuwa wanapata shida kama hizi; kweli kuna mechi ingekuwa inachezwa? Kama refarii angesikiliza mashabiki na wamiliki wa timu, kweli wangeweza kuchezesha mchezo wowote?

Tatizo la pili; ni Jeshi la Polisi. Sijasema tatizo ni Askari Polisi. Nimesema Jeshi la Polisi. Suluhisho langu kuhusiana na hili hapo kesho, likipokelewa na wenye kupokea na wakalifanyia kazi nawahakikishia kwa asilimia 90 litabadili kabisa mahusiano kati ya Jeshi na vyama vya upinzani na litatengeneza mazingira mapya kabisa ya kisiasa.

Itaendelea Kesho
Siku zote huwa nashindwa kukuelewa Mwanakijiji. Inawezekana una uelewa mdogo au unafanya makusudi kupotosha watu. Huwezi kuitenganisha tume ya uchaguzi ya Tanzania na utawala (Rais).
Hata kama Katiba na sheria zinasema haiwezi kuingiliwa na mtu.

Figisu figisu ilizofanya NEC ngazi ya Taifa hadi jimboni, ni ya makusudi kabisa kwa lengo la kuiwszesha CCM kushinda na wamefanikiwa.

Leo tunaomboleza kifo cha Akwilina kwasababu ya uozo wa NEC. Lakini hawa wote ni wateule wa Rais. Wanatekeleza maagizo tu
 
Naona mleta mada unazunguka mbuyu tu.
Tatizo kuu ni Magufuli. Narudia tena, tatizo kuu ni Magufuli. Jeshi la Polisi na Tume ya uchaguzi wanafanya huo upuuzi na uhuni wao hadharani kwa ujasiri na kujiamini kwa sababu wanajua wazi kabisa Magufuli yupo nyuma yao. Ndio aliyewatuma na ndiyye anayewalinda.

Tuchukulie kwa mfano; wewe ndio Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi halafu Rais Magufuli kasema alivyosema; ungefanya tofauti na wanalofanya hawa?
 
Yaani kurasa 77 za Mzee Mwanakijiji hili hakuliona au anajitoa fahamu?

Tatizo wengine mnafikiria vitu kama hivyo mimi navijali sana; naishi na Trump hapa na anasema mengi kweli.. Magufuli si mgeni kwa Watanzania; hakuna mtu ambaye alikuwa anamjua Magufuli kabla ya kuwa Rais anaweza kusema anashangazwa na kauli anazotoa; isipokuwa mtu mwota ndoto. Sijali sana maneno anayotoa Magufuli ambayo hayana msingi katika sheria na Katiba kwangu ni porojo tu za kuchangamsha genge. Ukichukulia kila kitu literally; mnaweza kujikuta kweli mnaanza kulima kwa meno kwa sababu Rais alisema akichaguliwa watu watalima kwa meno!
 
Siku zote huwa nashindwa kukuelewa Mwanakijiji. Inawezekana una uelewa mdogo au unafanya makusudi kupotosha watu. Huwezi kuitenganisha tume ya uchaguzi ya Tanzania na utawala (Rais).
Hata kama Katiba na sheria zinasema haiwezi kuingiliwa na mtu.
Hili linawezekana ni tatizo kwa baadhi yenu; siyo mimi ninayejaribu kutenganisha vyombo hivi; vimetenganishwa kwa makusudi katika Katiba. Watu wanapotaka wengine waheshimu Katiba na sheria ni lazima wajue kuwa sheria ni yote na Katiba ni yote.
 
Kama umelisikia na bado ulichokiandika kimetoka kwako au kuna mtoto katimia Simu au IPad yako ?
Kama ni wewe kweli umeandika basi
Umetumia moyo akili umemwachia mwanao
Zamani ulikuwa unaweza kujenga hoja; sasa chuki imeondoa uwezo huo?
 
Nakumbuka Rais wa nchi hii aliwahi kutamka hadharani ni namna gani alitamani angekuwa IGP

Kitu ambacho sikumbuki ni ikiwa Rais alitamka hayo baada ya kuona Jeshi la Polisi likishindwa kupambana na uhalifu kero na sugu dhidi ya raia na mali zao au baada ya Jeshi la Polisi "kushindwa"
kushughulikia watu!

Kuna kauli nyingine pia nakumbuka lakini wacha nijipe muda kukumbuka sawasawa!
 
Kuna watu wanasema ati kwa vile Rais kasema kauli zake basi watumishi wanaondoa ufahamu kabisa. Ilitarajiwa baada ya Rais kusema alichosema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipaswa kutoa maagizo ya kuwataka watendaji wote kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sharia na Katiba na bila upendeleo. Angewataka wahakikishe aliyeshinda kwa halali ndio anatangazwa.

Tumezoea kulea tabia za uzembe na watu kutozingatia maadili yao ya kazi ndio maana tunazitolea udhuru. Mtu amepewa majukumu na anajua majukumu yake halafu anasema "anaingiliwa". Hivi huko wanakojifunza, hawajifunza kujiuzulu? Ina maana Tanzania watumishi wote hawana ujasiri wa kusema "mimi hili sifanyi"? Au ndio watu wanasema "njaa" kwa hiyo njaa imewaondoa kabisa weledi?

Ukikubali hili; unafikiri itakuwaje?
Mzee sijui kama unaelewa top officials wa serikalini wavofanya kazi kwa hofu na kujipendezeka awamu hii. Vituko tunavyovishuhudia huku unatamani kulia na kucheka kwa wakati mmoja. Watu wako terrified, wako terrorized hadi mtu hata amuzi dogo tuu anawaza what if mkuu akija kuniuliza hapa... Yani siku hizi nyekundu inaweza kuwa njano mchana wa saa saba
 
Naona mleta mada unazunguka mbuyu tu.
Tatizo kuu ni Magufuli. Narudia tena, tatizo kuu ni Magufuli. Jeshi la Polisi na Tume ya uchaguzi wanafanya huo upuuzi na uhuni wao hadharani kwa ujasiri na kujiamini kwa sababu wanajua wazi kabisa Magufuli yupo nyuma yao. Ndio aliyewatuma na ndiyye anayewalinda.

Chunguza mwenendo na matamshi Magufuli kuhusu mwenendo mzima kuhusu siasa, upinzani, uchaguzi na vyombo vya dola na hapo utapata jibu kamili.

Kama Tume ya uchaguzi inaweza kufanya ushenzi wote ule, na bado Magufuli anakuja hadharani kupongeza washindi bandia na kuipongeza tume ya uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi ule 'vizuri', hapo unategemea nini?

Kama jeshi la Polisi linaweza kuua binti mwanafunzi hadharani na Magufuli anakuja hadharani kuwapongeza kwa kazi nzuri ya usalama, hapo nategemea nini?

Badala ya kuwafukuza kazi viongozi wote wa juu wa wizara ya mambo ya ndani na jeshi la polisi, Magufuli yuko busy kuizinisha ahadi ya milioni 80 ili kugharamia mazishi ya binti aliyeuwawa na polisi ili kuzima mjadala.
Nakumbuka hata Jecha alipongezwa hadharani....
 
Back
Top Bottom