KIDALI PO
Leo ni hoja hojani!
1. Jina la clinic ni lipi? Au aliyejaza hii hajui taratibu za hospitali? Au HAYUPO hospitali, kaijazia shambani?
2. Mtoto kazaliwa hospitali, ila hakuna jina la mhudumu. Au aliingia labor ward akajifungua huko mwenyewe mwenyewe?
3. Mtot hajulikani anapoishi, hata mzazi wa kiume hajulikani anapoishi... Hata kanisani hakujulikani ni eneo gani? Maana kama alipatikana chini ya madhabahu, basi hapo ndipo hom, ama? Au pale alipomtandikia mwanae, napo hapana jina?
4. Chanjo ni SIKU MOJA?? UUUUWI huyo mtoto hakufa? Nesi gani asojua muda wa chanjo jamani? Mbona mwadhalilisha hii taaluma?
5. Hivi huu mwandiko mbona ni wa mtu mmoja, kalamu nyeusi ile ile? Au siku hizi kuna restrictions kwamba LAZIMA kalamu nyeusi itumike kama vile mnajaza fomu za mkopo za HELSB?
Na huyu mjaza kadi, ina maana ni yeye pekee ambaye anamhudumia mama huyu? Au kwa vile mtoto katoka chini ya madhabahu? Yaani yeye kazi yake ni kumsubiri mchepuko wa Gwajima auhudumie?
6. Mtoto hana namba.. Huyu mtoto ni wa nchi gani? Kwamba hospitali alomzaa mwanae aidha ni mpyaaaaa, yaani huyu mtoto ni wa namba "sifuri"... Au kwenye hiyo hospitali alimozaliwa, kama ni kongwe, basi huwa hawajazi taarifa zozote za mtoto alozaliwa...
7. Kwa miaka ya karibuni, lazima baba wa mtotot ahudhurie kliniki au kuwe na barua toka kwa ofisi za serikali ya mtaa kumhusu huyo baba mzazi kama ni mume wa wenyewe. Nayo inatosha kabisa kujazia hizo taarifa ambazo HAZIPO. Nafikiri hii itafutwe
NIWASAIDIE
1. Kama ni kadi ya kweli watuambie hospitali ni ipi, waweke pia kielelezo cha register, siku huyu mama amepokelewa, muda, nk.
2. Iwepo kadi ya clinic ya mama mjamzito na records zake katika register book.
***Kadi ya mama ya clinic ina taarifa zote muhimu hasa tarehe ya mtoto kuzaliwa, maumbile, uzito, muda aliozaliwa, mhudumu na jina la hospitali
***Vitu hivi vinapatikana kirahisi, lakini register book sio rahisi uichakachue, maana ukitaja jina la Hospitali, na namba ikaonekana, taarifa kuzipata uhakiki ni rahisi sana... Ila kuhonga madaktari wampokee na kumfanyia registration mtoto feki ni ngumu....
***Inaelekea huyu alotoa wazo la kadi ya kliniki hajazaa, angekuwa ana mtoto asingefanya shudu hizi
***tafuteni kisa kingine, hiki mmekiharibu, hakiuziki
NB: SUALA LA MTOTO NI WA NANI HALINIHUSU NA SILIJADILI.
HAPA NIMEWEKA SAWA UJAZWAJI WA KADI YA KLINIKI, BASI
[emoji767]Happy J (BIBI)