Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Shirika la habari la jimbo la Florida limesema mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman amempigia simu Rais Donald Trump na kutoa rambirambi zake kwa familia na wahanga wa tukio la ufyatuaji risasi lililofanyika katika kambi ya wanamaji ya Florida hapo jana.
Mwanamfalme huyo pia amemuhakikishia Rais Trump kuwa Saudi Arabia itatoa ushirikiano unaotakikana kwa Marekani na itatoa taarifa zozote zinazohitajika katika uchunguzi wa tukio hilo.
Wachunguzi wanaamani kuwa luteni wa jeshi la angani la Saudi Arabia alifanya shambulizi hilo pekeyake alipowauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine wanane huko Pensacola, Florida.
Kulingana na shirika la upelelezi la Marekani FBI, mwanajeshi huyo wa Saudi Arabia aliuwawa baadae kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi.