Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 93
- 238
Mwanamitindo bingwa duniani Naomi Campbell sasa ndiye balozi wa ‘Magical Kenya International’, Wizara ya Utalii imethibitisha.
Makubaliano ya kuwa balozi yamefanikishwa na Mhe. Waziri wa Utalii Najib Balala leo jijini Mombasa.
Kenya inatazamia kujinadi kama sehemu na nchi bora zaidi ya kutalii katika bara la Africa. Ikumbukwe mataifa mengi duniani sasa hivi yapo mbioni kuendeleza uchumi ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020, shughuli za Utalii zilitatizika know kutokana na janga la virusi vya Corona.
Akihutubia wanahabari, Mhe Waziri Balala amesema ni bahati kubwa kwamba Campbell ameridhia kuwa balozi wa ‘Magical Kenya International’ hususan katika katika kipindi ambapo nchi zinajizatiti kufufua uchumi.
“Tunashukuru Sana kwa bahati hii kubwa ya kumnasa Naomi. Naamini atatangaza uzuri wa taifa letu” amesema Waziri Balala.
Kwa upande wake Naomi Campbell amesema kwake ni heshima kubwa pia kupata nafasi ya kutangaza Kenya.
“Kenya bila shaka ni sehemu pazuri. Sote tunafahamu hilo. Ni wakati mwafaka sasa kuwakumbusha watu kote duniani kuwa wakitaka kutalii wazingatie kutalii Kenya” amesema Campbell.