Mwanamke Abadilishana Watoto Wawili Kwa Kasuku!

Mwanamke Abadilishana Watoto Wawili Kwa Kasuku!

Micheweni Pemba

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Posts
351
Reaction score
179
Wakubwa Shkamooni wadogo Habari zenu.
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametupwa jela miezi 30 na kufanyishwa kazi ngumu baada ya kukiri kubadilishana watoto wawili kwa ndege aina ya Kasuku Kishungi.

Donna Louise Greenwell mwenye umri wa miaka 52
alipatikana na hatia ya kufanya biashara ya kuuza watoto wawili kwa kubadilishana kwa ndege aina ya Kockatoo (Kasuku Kishungi) pamoja na pesa dola 175.

Donna amehukumiwa kwenda jela miaka 15
pamoja kazi ngumu kwa kila kosa moja alilokiri la kuuza watoto na ataanza kutumikia adhabu yake septemba 25 mwaka huu.

Donna anatuhumiwa kuwauza watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.

Donna aliwauza watoto hao baada ya kukubali kupokea malipo ya kasuku kishungi mmoja na pesa kiasi cha dola 175.

Watoto hao walikuwa si wa Donna. Wazazi halisi wa watoto hao walimuachia Donna watoto hao awalee.


"Kweli dunia ina vituko wengine tunaona wanaiba watoto huyu nae anauza watoto kwa kupewa kasuku na dola 175 hahaha akili ni nywele kil amtu ana zake".
Hayo ni maneno yaliyolalamikiwa na mdau mmoja wa sheria aliyekuwa akilalamika peke yake pembeni.
jee wewe una maoni gani?.
 
Back
Top Bottom