Mwanamke afikishwa Mahakamani kwa kumnajisi mwanafunzi

Mwanamke afikishwa Mahakamani kwa kumnajisi mwanafunzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanamke mmoja alifikishwa katika mahakama ya Milimani Jumatano Januari 30, kwa mashtaka ya kumnajisi mvulana wa darasa la nane kwenye seli ya polisi.

Mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 23 alikuwa amezuiliwa pamoja na mvulana huyo kwenye seli moja wakati alitekeleza kitendo hicho.

Hata hivyo, Naomi Nechesa Sanya alikanusha madai ya kushiriki ngono na mvulana mwenye umri wa miaka 15 kwenye seli Jumapili Januari 27.

Kufuatia kisa hicho, maswahili yaliibuka ni vipi mvulana huyo mwenye umri mdogo alipatikana kwenye seli hiyo ikizingatiwa kwamba angezuiliwa kwenye makazi ya watoto.

Kulingana na mwendesha mashtaka ya kitaifa Kennedy Panyako, mvulana huyo angezuiliwa tu kwenye seli hiyo kwa sababu hangezuiliwa kwenye seli ya wanaume wazima.

Mvulana huyo alikamatwa baada ya madai alikuwa akitumia mihadarati.

Nachesa ambaye alikuwa amezuiliwa kwa madai ya mauaji, aliitaka mahakama imuachilie huru ili aweza kuenda nyumbani kumnyonyesha mwanawe mwenye umri wa miezi 11.
 
Mwanamke miaka 23 na mvulana miaka 15, hivi walimu kama hawa walikua wapi enzi zangu shuleni, maana ningemfahamu mwalimu wa kihivi, ningekua napita pita kwenye kumi na nane zake.
 
Haya mambo yanatokea sana na effect yake kwa mtoto wa kiume ni sawa na ile anayopata mwanamke lakini jamii huwa inapotezea. Mtu kama R Kelly yalimfika haya akiwa mdogo matokeo yake amekuwa a freak weirdo.
 
Back
Top Bottom