Mwanamke akata uume wa mmewe

kaburunye

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2010
Posts
672
Reaction score
79
MKAZI wa MKAZI wa Kiwalani, Bi. Halima Thomas (28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka ya kumkata uume mume wake.Mwanamke huyo alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ulidai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo Agosti 27, mwaka huu saa 6 usiku, Kiwalani Yombo jijini Dar es Salaam.

Aliileza mahakama kuwa kwa makusudi mshtakiwa alimkata uume mume wake (jina tunalihifadhi) kwa kutumia kisu na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.

Baada ya kusomewa mashtaka, mshtakiwa alikiri kosa hilo na mahakama inasubiri taarifa kutoka kwa daktari ili imsomee hoja za awali.

Nje ya mahakama, mshtakiwa alidai kuwa amefanya hivyo kwa ajili ya kumkomesha mume wake ambaye anadai kuwa amemwambukiza virusi vya Ukimwi.

"Nasikitika kwa kumkata kidogo ule uume, ningejua ningeumalizia kabisa ili usifanye kazi tena kwani ataendelea kusambaza Ukimwi kwa wanawake wengine," alidai mshtakiwa.

Mshtakiwa yupo rumande na kesi itatajwa tena Oktoba 12, mwaka huu.Kiwalani, Bi. Halima Thomas (28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka ya kumkata uume mume wake.Mwanamke huyo alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ulidai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo Agosti 27, mwaka huu saa 6 usiku, Kiwalani Yombo jijini Dar es Salaam.

Aliileza mahakama kuwa kwa makusudi mshtakiwa alimkata uume mume wake (jina tunalihifadhi) kwa kutumia kisu na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.

Baada ya kusomewa mashtaka, mshtakiwa alikiri kosa hilo na mahakama inasubiri taarifa kutoka kwa daktari ili imsomee hoja za awali.

Nje ya mahakama, mshtakiwa alidai kuwa amefanya hivyo kwa ajili ya kumkomesha mume wake ambaye anadai kuwa amemwambukiza virusi vya Ukimwi.

"Nasikitika kwa kumkata kidogo ule uume, ningejua ningeumalizia kabisa ili usifanye kazi tena kwani ataendelea kusambaza Ukimwi kwa wanawake wengine," alidai mshtakiwa.

Mshtakiwa yupo rumande na kesi itatajwa tena Oktoba 12, mwaka huu.

MY TAKE: Wanaume mnaoendekeza infedility kaane chonjo. Kuna siku mama watoto ataamua atoe hio kitu inayokusumbua kutoka nje ya ndoa ukose jumla kabisa.
 
Na yeye akifanya infidelity atakatwa kitu gani sasa?
 
duuuuu anakata kifanyio

Duh hapo mkuu usiombe ikutokee,mimi nilikuwa na wangu basi siku moja akanifumania, weeeeeeeeeh,nilikoma maana alipomaliza kumshughulikia mgoni wake akaniambia na wewe nakusubiri ulale tu nikukate hicho kinachokusumbua tukose wote.Basi nilihama chumbani wiki nzima na hata nilivyorudi chumbani sikulala vizuri karibu wiki tatu maana mwenzangu akigeuka tu najua eeenhee anatafuta kisu na hiyo ilikuwa ni hofu tu sasa angekikata kweli sijui ingekuwaje?Nampa pole huyo mjomba hii infii hii watatuua tu.
 
Duu hako katabia naomba kasiene maana tutabakiwa na vibutu
 
nako huko zimbabwe mwezi uliopita kuna bibie
nae aliamua kukata dhakari ya mumewe na baada
ya hapo akamchuma moto huyo husband. jamaa alikuja
kata roho hospitali baada ya siku mbili.
 
MY TAKE: Wanaume mnaoendekeza infedility kaane chonjo. Kuna siku mama watoto ataamua atoe hio kitu inayokusumbua kutoka nje ya ndoa ukose jumla kabisa.
kweli aisee, hata mimi huwa nasema kwamba tukiendekeza infii tutakatwa hiyo njuruu... lakini pia huwa najiuliza, na mamaa atatumia ipi akipata hanjam?
 
Sasa akishaikata jamaa ni kweli hatofanya tena nje. Je sasa ndio atafanya ndani? Mama akijisikia nini kitamfanya? Au ndio itakuwa zamu yake ya kutoka kwa mijamaa sasa? Think b4 u act!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…