Mwanamke akipewa pesa husifia chochote

Mwanamke akipewa pesa husifia chochote

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
Yeaaah, mwanamke akishapata pesa tu kutoka kwa mwanaume huweza kusifia kila kitu.
Utafiti usio rasmi uliofanywa na Mimi mende msafi umebaini kuwa ukiishampa pesa mwanamke, mwanamke huyo anaweza kukusifia kwa lolote lile hata katika mapungufu yako.
Iko hivi, mimi siyo MTU mwenye kipato kikubwa kwa hiyo hata sehemu niliyopanga si nzuri. Lakini nimejaaliwa roho ya kuhonga kiasi kikubwa cha kipato changu hivyo kufanya niweze kupita na wanawake wengi sana.
Na kwa kupitia matukio yafuatayo napenda kudhibitisha utafiti wangu.

1: mmoja aliwaona mende wakubwa chumbani kwangu akasema "waaaaoooh, mende wako wana rangi nzuri. Kama chocolate vile"

2: mwingine aliona panya akastuka kisha akasema "hee baby, umemuona panya aliyekatiza hapa? Ana masikio mazuri kama sungura vile. Next time nikija si utanigeia mmoja na mimi nikamfuge. Si eti honey"

3: mmoja aliliona shuka langu lililotoboka toboka akasema " mmh we mbunifu, unajua hili shuka ni mult purpose eeeh. Unaweza tumia kama shuka na pia kama neti.

NB kila anayekuja geto huwa hataki kuja tena, sijajua kwa nini.
 
Hivi hizo sifa au wanakukejeli? Hao wamekudharau kiaina lakini mwenyewe umeona umesifiwa. Chumba kina Panya, mende na shuka la kolomije hao mademu wanatokea wapi? Ulambo. [emoji12][emoji1][emoji111]




Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Ngoja niende kwa pusha nkamuulize km anayo hii kitu ya Afghanistan..
 
Utasikia..."hello handsome"


Wakat ukijiangalia kwny kioo unacheka mwnyw
 
Back
Top Bottom