umenena vemaWote wawili!
Wote wawili!
Hivi katika jamii nani ana set standards za hicho kinaitwa 'maadili'?
Who are we to judge other peoples life styles?
Pilipili usiyokula yakuwashia nini?
Mtu yuko kwake na wanae wanakula,wanavaa ,wanasoma,kwenye bembea anawapeka,always she/he is there for them,sisi wengine hizi kelele ni za nini?
Watoto wangapi wanalelewa katika so called perfect arrangement ya baba na mama under one roof na unakuta baba wiki haoni watoto ni kuondoka alfajiri kurudi usiku mama mlevi,baba na mama wanapigana mbele ya watoto na matusi kwa kwenda mbele, etc.
Wana mmu jamani live and let live,tuache kuwa tunahukumu maisha ya watu,afterall kitanda usicholalia...
matatizo ya kutaka unavyoishi wewe ndo kila mtu aishi hvyo. Wanasahau kila mtu anaishi vile atakavyo c kwa kuangalia fulani au kikundi fulani kinavyotaka.
Yaleyale ya kusema kuoa/kuolewa ni heshima, wakati kinacholeta heshima ni tabia ya mtu. Ukiwa kwenye ndoa wakati ni mzinzi, mlevi, mala**a, heshima iko wapi?
mi naona ni fashion tu kwa vijana wengiSwali la msingi...kuoa ni maadili?...
Mwanamke ambae Hajaolewa at age 28+ bila sababu za msingi.
Mwanaume kama hajaoa 35+ bila sababu za msingi...
- Anaonekana kama alikua wakujirahisi hasa kama ana zaidi ya mtoto mmoja baba tofauti.
- Anaonekana kama alikua anachagua saana wachumba mpaka kashangaa tu umri umeenda.
- Anaonekana ana kasoro hasa mwilini (hata awe mzuri vipi) hasa maeneo husika.
- Anaonekana kama vile sio wife material, tena usiombe ni msomi ambae ni independent.
- Akiwa na watoto wa baba mmoja anakua defined kama nyumba ndogo...
- Ukweli ni kwamba pamoja na kusema heshima ipo, heshima sio genuine tofauti na rika hilo mwenye mume ama aliewahi olewa.
Take NOTE: Nimeongelea wale ambao kabisa hawajawahi Oa/Olewa. ALAFU Tusidanganyane Jamani, Ndoa ina Heshima yake kubwa saana katika Jamii na macho ya Jamii.. Ni moja ya taasisi ambayo inamfanya mtu aheshimike, hata hivo wale ambao hawakubaliani na maneno yangu... sio lazima.
- Anaonekana hapendi majukumu ya kulea familia - hasa kama ana watoto.
- Asipoonekana na wanawake mara kwa mara huonekana *******... ama kua na matatizo fulani, saa ingine hata kuzushiwa shoga...
- Anoanekana ni player, tena mara nyingi na vibinti vidogo... (jamaa wa namna hii hupoteza hata marafiki) maana wanajua tabia zake, hawamtaki karibu na dada/wake/watoto zao..
- Anaonekana si kamilifu mbele ya wanaume wenzake hata kama anabadilisha wanawake kama nguo...
Ni heshima iwapo tu wahusika nao wanaiheshimu hiyo ndoa....otherwise ni udanganyifu mtupu.
Kiukweli Lizzy Wanandoa wengi wanakaa katika ndoa zao siku hizi out of obligation rather than Love, Hio imefanya kua heshima ya Spouses dhidi ya ndoa zao zishuke kwa kiasi kikubwa... Ila kumbuka kua as much as walooana ni wawili, hawaishi in isolation hawa watu, jamii nayo inawaangalia pia kama wanandoa. Na wanajamii hata hua hawaangaliag logic (kweli ni kitu cha ajab - yet funny in a sad way) Hawajali kwamba hampendani, hawajali kua mmoja ni cheater or both, hawajali kua mmoja hulala constantly nje... Wao wanachoona ni kua tu wale pale (hio couple ni wanandoa.. baas)...
Hivo basi tukiangalia hio ndoa kwa macho ya jamii nzima (tuache logic) wanaona ni ndoa na watawaheshim as a couple... BUT nyie wahusika sasa kama Mke ama Mme ndo mwaweza sema accurately kama kuna ndoa hapo ama lah! tegemea na kama kila mmoja aheshimu hio ndoa ipasavo.
Ndoa si fashion. Si mpango wa jamii moja tu. Si mpango wa dini moja au mbili. Si mpango wa kabila au tamaduni moja. It is universal culture. Nadhani ukikosa kuwepo kwa sababu zisizo za msingi, wewe ndo mwenye matatizo.
Waulize watoto waulize watoto wanaolelewa na mama zao tu, wanavyotamani wangekuwa na baba zao, ni hivyo hivyo wanalelewa na baba zao wakati mama zao wako hai.
Si jambo dogo, wengi lina waathiri kisakolojia.
Halafu, asilimia kubwa ya wanadamu wa kawaida hutamani kuoa au kuolewa, wanapokuwa wamekosa au wamekosea njia ndo husema ndoa kitu gani. Hapo yanakuwa maneno ya mkosaji.
Unayosema ni kweli kabisa....ila mimi nlikua namaanisha HESHIMA ya kweli, wanayostahili wanandoa achana na hii ya kinafiki.
Binafsi nashindwa kuelewa nia na maana ya kuheshimu ndoa tu ilimradi ndoa wakati baadhi ya wenye hizo ndoa maisha wanayoishi hayana cha maadili wala nini.Ifike mahali jamii ianze kuangalia mambo kwa undani badala ya kupaka hata yale maovu rangi za kupendeza na kujaribu kuwafanya wale wanaoishi maisha yaliyonyooka (japo tofauti na matarajio/matakwa ya jamii) wajisikie vibaya na kujihisi ni wakosaji.