Hi Mozambiqueone
Ninavyofaham mimi; Kama mwanamke atawekewa Norplant akiwa kwenye hedhi (kati ya siku ya kwanza hadi ya tatu hivi) anaweza kuendelea na tendo la ndoa baada ya hedhi bila wasiwasi wa kupata ujauzito; Tofauti na hapo, Madaktari wanashauri asubiri kwa muda wa siku saba (7) ndio huwa tayari kwa kazi ilkiyokusudiwa.
Napendekeza wakati mwingine uwe mdadisi kwa kuuliza haya maswali kwa Daktari aliyehusika kutoa hiyo kinga
Kumbuka: Norplant kazi yake ni kuzuia ujauzito tu; kama kuna magonjwa mengine yataendelea kuambukizwa