pole sana,
1-Ila naamini umemkaribisha huyo mgeni pasipo kukubaliana na mkeo,jambo ambalo kama wana ndoa haupaswi kufanya hivyo USIRUDIE TENA KULETA UGENI PASIPO BARAKA ZA MKEO,ksb maamuzi ya kupokea wageni lazima mkubaliane wanandoa wote ukizingatia pia kuwa hata bajeti hua inabadilika pindi mgeni anapokuwepo.
2-Pia huyu mgeni alipofika hapo nyumbani alibehave vipi kwa mkeo, manake kuna wageni wangine japo siyo GFriend kama ulivyosema lakin anaweza kuwa ameonesha dharau kwa mkeo au amejishaua weee kiasi ambacho kimemkera mkeo,manake wageni wengine wakiingia majumbani mwa watu hayo mashauzi yao mmmhh ni karaha tupu.
3- Wala usimfiche huyo mgeni wako mwambie kinachoendelea kati yako na mkeo kama ni mstaarabu basi ataondoka/ kama siyo mstaarabu wewe mwondoe kwa ustaarabu aende Gest HSE akafikie huko mpaka apate hapo atakapopata pa kuishi.
4- Huyu mkeo SIMUUNGI MKONO KUONDOKA HAPO HOME japo kakereka na huo ugeni,ksb kuondoka kwake HAKUTATUI TATIZO BALI NI KUONGEZA TATIZO, lakin kwa vile kaondoka na ili na wewe kuonesha kuwa kweli UNAMPENDA,UNAMTHAMINI,UNAMJALI,UNAMHITAJI, KUONESHA KUWA MKEO NI MUHIMU NA BORA ZAIDI KULIKO huyoooo mgeni wako basi MTAFUTE MKEO ,MWOMBE MSAMAHA ILI MAISHA YENU YAENDELEE VIZURI KAMA WANANDOA. Mgeni asiwe chanzo ya KUVUNJIKA KWA NDOA YENU. Ila pia jaribu kumsoma mkeo je ni mke anayependa wageni??, na kama ndiyo anapenda je wageni wa aina gani??,na kama ni kati ya wale wasiopenda wageni basi kama unampenda pia una uamuzi wa kuishi naye hivyohivyo kwa kutopokea wageni au laa. Ila kama hapendi wageni basi HAKIKISHENI NA NYIE MSIWE WAGENI MAJUMBANI MWA WATU,lol.