Ni wanawake wachache sana tena waliobarikiwa na Mwenyenzi Mungu ambao wanaweza kubalance success na maisha ya ndoa/family. Mfano mdogo tu angalia ni wanawake wangapi ambao wapo kwenye ngazi za juu kisiasa ambao familia zao pia zimestawi? Sio lazima wawe wametengana na waume zao lakini wanakuwa ndoa zisizo na furaha, sio wote lakini wengi wao wameathirika kindoa kutokana na mafanikio yao. Sijui wanaJF wenzangu mnalionaje hili?
[
QUOTE=JS;1013865]Wandugu za leo,
Hivi ukikutana na mwanamke umempenda na unatamani awe wako wa milele (kumuoa) lakini unakuta bahati nzuri (au mbaya kwa wengine) huyo mwanamke yuko safi kimaisha kazi nzuri kama pesa anazo kama mali anazo pia (sio hawa wamama watu wazima hapana wadada tu wenye umri unaofaa kuolewa) utamuoa hata kama wewe huna thamani ya kiuchumi aliyo nayo?
kwa nini nimeuliza hivi, kwa sababu katika mazungumzo ya kawaida tu jana kuna rafiki yangu akaniambia watu wataogopa kutangaza nia kwangu nikiendelea kujijenga kimaisha and it got me thinking.
Sasa wanaume utamuoa tu huyo dada hata kama wewe hali yako si fresh? na wadada utakuwa bread provider kwa huyo mumeo? mapenzi yana nafasi yake na pia uwezo kiuchumi una nafasi. zamani haikuwa hivi lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele mambo yanabadilika[/QUOTE]