MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Kuna tetesi kwamba yule mwanamke mwenye asili ya kiasia, miaka 23, ambaye yeye na mumewe, miaka 23, amefariki dunia baada ya kuteswa na askari polisi na magereza akiwa mahabusu jijini Dar es Salaam, kwenye mojawapo ya magereza ya Keko, Segerea au Ukonga, ambapo alikuwa amewekwa chini ya ulinzi.
Inadaiwa kwamba, katika kujaribu kupata habari zaidi kutoka kwa mwanamke huyu kijana kabisa, ambaye alionekana kuwa na hofu iliyozidi kipimo alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, askari hao walitumia njia ambazo zimepigwa marufuku katika upelelezi, njia ambazo hata kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeharamishwa. Njia zinazosadikiwa kutumiwa ni pamoja na matumizi haramu ya umeme, ambao ulitumika kumpiga shoti mwanamke huyo.
Chanzo cha habari hizi ni ndugu wa kiume wa mfanyabiashara aliyeuwawa na wanandoa hao, ambaye amesikika na kunukuliwa akipasha habari za kufariki kwa mwanamke huyo, huku akidai kwamba kuna njama za kuficha ukweli kuhusu kifo cha mwanamke huyo kwa kuupeleka mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kuweza kudai kwamba mwanamke huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Tunawaomba walio na habari zaidi watusaidie kupata ukweli wa jambo hili, kwani ni aibu. Mara nyingi watu ambao bado hawajathibitika kuwa na hatia wamekuwa wakifariki kwa kipigo na mateso, ama wakiwa mikononi mwa polisi, ama wakiwa mahabusu. Tanzania ni nchi iliyoweka saini kwenye Mkataba wa Haki za Kibinadamu wa Geneva (Geneva Convention on Human Rights). Huu ni ukiukwaji wa haki za kibinadam, ambazo zimeainishwa kwenye katiba.
Tuutafute ukweli ili haki itendeke. Tusikubaliane na watakaojaribu kuuficha ukweli.
./Mwana wa Haki