Mwanamke auliwa na mumewe akiwa usingizini chanzo mgogoro wa kifamilia, Katavi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Getrude Silivesto miaka 38 mkazi wa kijiji cha Kaulolo Kata ya Nsekwa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki dunia kwa kuchomwa na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali sehemu ya mbele ya sikio la kushoto na upande wa shingoni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema tukio hilo la kusikitisha limetekelezwa na mme wake Talisiswusi Salvatory miaka 42

Kamanda ngonyani amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia wa muda mrefu huku akibainisha tukio hilo limetokea Majira ya Saa Moja Asubuhi kuamkia Julai 2,2025

Amebainisha kuwa tukio hilo limetekelezwa na mme wake huyo wakati mke wake akiwa amelala na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali

Kwa mujibu wa Kamanda Ngonyani mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo katika kituo cha polisi inyonga Wilala ya Mlele kwaajili ya mahojiano zaidi kuhususiana na tukio hilo na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani

Katika hatua nyingine Ngonyani ametoa wito kwa wananchi hususani wanafamilia wanapokuwa na changamoto za ndoa kutumia dawati la polisi la jinsia ambalo linahusika na masuala ya kifamilia pamoja na viongozi wa dini kwenye maeneo yao ili kuepusha kujichukulia sheria mkononi

Chanzo: EAST AFRICA TV
 
Ukute walishirikiana vizuri tuu umesinzia bisu la tumbo jamani 😭
 
Watu wa mikoani mpo serious sana na nyege
Hiyo mivyakula mnayokula kula inawatia nyege
 
Nimesikitika sana mkuu na ili masikitiko yangu yaishe naomba no ya simu ya huyo pongo wa nyuma ya SACP K.C. NGONYANI.
 
Bado tu hawajalinyonga hilo liuaji, walinyonge taratibu taratibu hadi alilie kifo yeye mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…