Mwanamke kufukua makaburi bila sababu inatokana na nini?

Mwanamke kufukua makaburi bila sababu inatokana na nini?

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,952
Kuandika Uzi wa mapenzi asubuhi subuhi haimaanishi kwamba hatujengi Taifa. LAA!

Muhali gani wapendwa? Nawaombea muwe na afya njema.

Ni swali fupi tu
JE NINI KINAFANYA MTU KUFUKUA MAKABURI (MAMBO MAOVU) YA ZAIDI YA MIAKA MIWILI NYUMA?

Mpenzi wangu na mama mtoto wangu ambaye yuko mbali na mimi kwa sasa, Jana tulijikuta katika malumbano makubwa baada ya yeye kuanza kuniuliza kuhusu mambo flani mabaya ambayo niliyafanya Miaka ya nyuma.

Jambo lenyewe ni kwamba alinikuta na dalili na nyaraka zote zinazoonesha kuchepuka. (Nilikataa kata kata ingawa ilikuwa kweli)

Lakini mambo yalikwenda na yakaisha kwa amani na upendo ukaendelea.

Ajabu ni kwamba jana baada ya kukosa cha kuzungumza akaanza kunikumbusha yale mambo. Na sio kunikumbusha tu bali alijipanikisha baada ya kukumbuka lile tukio kana kwamba limetokea sasa hivi.

Nikamuuliza kwani mbona masuala yalishaisha? Au Kuna nini tena ?

Nikaona huku sasa ni kuzoeana vibaya. Nikaanza kumfokea na kuanza kujibizana hadi usiku mkubwa. Nikampiga biti na kumwambia kwamba KAMA UMECHOKA KUWA NA MIMI JIKATAE MAPEMA KUNGUNI WEE!

NIKABAKI NA MASWALI HAYA!

1. Hisia zake zimempotosha kwamba kwa sasa nachepuka kwa sababu niko mbali naye?

2. Amepata baharia mpiga makasia sasa ananikumbusha kwamba anauliza?

3. Amenichoka?
4. Kuyumba kwa uchumi kumempagawisha?
5. Mabadiliko ya hormone kwa kuwa ana muda mrefu hajafanya mapenzi? (Kwa MUJIBU WA imani yangu[emoji1])

6. Amechoshwa na kasumba zangu

Au nini shida?

NB
Sharauti sana kwa wanangu wote mlio oa ama kuishi na Mwanamke kwa muda mrefu.
 
Ni kawaida sana mtu kukumbuka matukio, maana vidonda hupona ila makovu wakati mwingine hayafutiki,

Inshu kubwa ungevunga tu kiume ukamwambia yamepita na na kumtaka radhi kidg walau yangeisha kwa Amani, maana wakati mwingine ni bora kuepusha malumbano, maana kama ni mke na uko mbali nae aisee sio nzuri kupishana kauli sababu anawezajikuta anauza mechi kwa boya anayem'bembelezaga
 
Kwanza nataka ujue kua uanaume ni kung'ang'ana. Hata kama umeshikwa na sms kataa sema siyo yako yaani hata iweje, na ndiyo maana wanaume tuna wale washkaji ambao likitokea la sms unasema hii ni ya fulani.

Na akipigiwa hakatai.

Ila mshkaji wa hivi hatakiwi mtu wake na mtu wako wajuane.

Pili kwakua uanume ni kusaidiana nataka nikwambie kwamba huyo ataendelea kukunyanyasa juu ya hilo swala mpaka upate dawa yake.

Dawa yake, nipe namba yake. Niambie muda gani upo home nampigia najiongelesha ni mpenzi wake na kila kitu. So na wewe utapretend kununa. Akianzisha mada ya huyo mchepuko we unaanzisha mada yangu
 
Ni kawaida sana mtu kukumbuka matukio, maana vidonda hupona ila makovu wakati mwingine hayafutiki,

Inshu kubwa ungevunga tu kiume ukamwambia yamepita na na kumtaka radhi kidg walau yangeisha kwa Amani, maana wakati mwingine ni bora kuepusha malumbano, maana kama ni mke na uko mbali nae aisee sio nzuri kupishana kauli sababu anawezajikuta anauza mechi kwa boya anayem'bembelezaga
Aisee
 
Kwanza nataka ujue kua uanamue ni kung'ang'ana. Hata kama umeshikwa na sms kataa sema siyo yako yaani hata iweje, na ndiyo maana wanaume tuna wale washkaji ambao likitokea la sms unasema hii ni ya fulani.

Na akipigiwa hakatai.

Ila mshkaji wa hivi hatakiwi mtu wake na mtu wako wajuane.

Pili kwakua uanamue ni kusaidiana nataka nikwambie kwamba huyo ataendelea kukunyanyasa juu ya hilo swala mpaka upate dawa yake.

Dawa yake, nipe namba yake. Niambie muda gani upo home nampigia najiongelesha ni mpenzi wake na kila kitu. So na wewe utapretend kununa. Akianzisha mada ya huyo mchepuko we unaanzisha mada yangu
Akirudi nitalifanyia kazi hili aisee
 
Hii ni kweli, nimeexpirience kwa wife, utaskia "usizanshie nimesahau Mambo yako, Sina chuma kifuani, nina roho ya Nyama" (Kwa lafudhi ya kikaskazini)

Hapo unakuta Mambo yalitokea 2014.
Ha ha ha kabisa aisee
 
sawa usivisahau, lakin kuja kuviongea tena after 2yrs Ni ujinga sistaa
Bado hujawajua wanawake vizuri Mkuu.

Wewe unadhani hata uamuzi wa kuchomana na petrol ni matokeo ya ugomvi wa muda huo huo?

Mimi nishawahi kupigwa tukio na mchepuko nilioachana nao karibu miaka miwili Nyuma, Tukio lilibadilisha Kila kitu kwenye maisha yangu mpaka leo bado sijacover damage za Hilo Tukio na unaenda mwaka wa 5 Sasa.

Toka anipige Tukio huyo Mchepuko, Nilimind sana, na mwezi mzima baada ya Tukio ningekutana nae huyo Mchepuko nadhani leo ningekua jela.. Nilipata hasira sijawahi kupata toka nipate akili.
 
Bado hujawajua wanawake vizuri Mkuu.

Wewe unadhani hata uamuzi wa kuchomana na petrol ni matokeo ya ugomvi wa muda huo huo?

Mimi nishawahi kupigwa tukio na mchepuko nilioachana nao karibu miaka miwili Nyuma, Tukio lilibadilisha Kila kitu kwenye maisha yangu mpaka leo bado sijacover damage za Hilo Tukio na unaenda mwaka wa 5 Sasa Toka anipige Tukio huyo Mchepuko, Nilimind sana, na mwezi mzima baada ya Tukio ningekutana nae huyo Mchepuko nadhani leo ningekua jela.. Nilipata hasira sijawahi kupata toka nipate akili.
Siku MOJA utuelezee hili.
 
Hii ni kweli, nimeexpirience kwa wife, utaskia "usizanshie nimesahau Mambo yako, Sina chuma kifuani, nina roho ya Nyama" (Kwa lafudhi ya kikaskazini)

Hapo unakuta Mambo yalitokea 2014.
Wanawake huwa hatusahau ni vile huruma ukiruhusu serious ndo waweza ua kwa petroni kama Neema au kufanya jambo baya.
 
Back
Top Bottom