Nina rafiki yangu wa karibu ameoa hivi karibuni alikuja kuniomba ushauri kwa vile nipo kwenye ndoa yangu kwa zaidi ya miaka 10. Akanieleza kuwa mke wake ana tatizo la kutokwa majimaji yenye harufu kali wakati wafanyapo tendo la ndoa. Aidha, alisema yapata mwaka sasa, mke wake huyo amewahifanyiwa operation chini ya kitovu iliyotokana na tatizo la uvimbe kwenye mirija ya uzazi.
Wanajamvi naomba wenye majibu ya kitaalam ili tuweze kumsaidia rafiki yangu.
Ikiwa si suala linalohusiana na usafi, aende kuwaona madaktari wa magonjwa ya wanawake. Pale namanga mbuyuni kuna Maria cliniki ya profesa Mgaya.