Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWANAMKE MWANAMAPINDUZI ANAINGIA DAR ES SALAAM
Nifuatilie hapa kwangu barzani kwa simulizi za kitabu hiki ingawa ikiwa ulikuwa unapita ukurasa huu ushanisoma mara tatu nikikieleza kitabu hiki.
Hii sasa ni makala ya nne.
Wa kulaumiwa si mie bali Biubwa Amour Zahor na Zuhura Yunus.
Kitabu hiki kinanigusa kwa njia nyingi tofauti.
Kwanza kama mwanafunzi wa historia ya Zanzibar.
Pili kama mtu niliyeshiriki kama Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany mwandishi wa kitabu mashuhuri, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," kitabu kinachoaminika kurekebisha mengi katika kuiandika historia ya Zanzibar kama inavyostahili kuandikwa.
Kitabu hiki cha maisha ya Biubwa kinaongeza mengi katika kuijua zaidi historia ya Zanzibar.
Tatu na hili kwangu limenistaajabisha kama mwandishi ni huku kuwakuta ndani ya kitabu hiki wametajwa watu ninaowafahamu kwa karibu na wengine kwa mbali, wengine wako hai na wengine wameshatangulia mbele ya haki.
Wengine tumefahamiana hapa nyumbani na wengine nje ya Tanzania.
Historia ya Zanzibar kwa wengi ni historia ya damu, majuto, majonzi na kumbukumbu mbaya.
Mwezi wa Ramadhani niko Zanzibar inakaribia Maghrib nimesimama pembeni ya ufukwe jirani na hoteli niliyofikia naangalia wavuvi wanarudi kutoka baharini bila shaka wanaharakisha kuwai adhana.
Kanijia kijana mdogo pale nilipokuwa kanitolea salaam nimemwitikia.
''Nadhani wewe ni Mohamed Said,'' kijana kaniuliza.
Tukaanza mazungumzo kijana akaniambia kuwa ananisoma sana.
''Kuna makala uliandika kuhusu mzee moja Pemba aliyepigwa viboko hadharani.''
Kijana akanyamaza kidogo macho anaangalia chini mchangani aliponyanyua kuniangalia usoni akasema, ''Yule mzee ni babu yangu mzaa baba.''
''Pole sana ndiyo niliandika kisa kile babu yako hakuweza kutembea baada ya kile kipigo ilibidi abebwe kurudishwa nyumbani na kwa aibu kuona kafedheheshwa kiasi kile hakutoka ndani katoka nje akiwa ndani ya jeneza kwenda kuzikwa."
Tulisimama pale kimya.
Sote hatukuwa na la kuzungumza simanzi zimeturejea kama lile jambo limetendeka jana.
Huyu mwanamapinduzi aliyefanya kitendo kile tukifahamiana lakini kabla sijakijua kisa hiki haikunijia kuwa kwa namna ile nilivyokuwa namuona msikitini haikunipitikia kuwa angeweza kufanya yale.
Labda ni hamasa ya mapinduzi na changamoto zake.
Hii ndiyo historia ya Zanzibar ninayokutananayo kote ninakopita ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.
Lakini kila jambo lina pande mbili.
Hoja ya upande wa pili ni historia ya utumwa.
Huuliza.
Utumwa uliotoweka vizazi na vizazi ndiyo hadi leo?
Turejee kwenye kitabu chetu.
Inanistaajabisha kuwa kitabu hiki kimenitajia watu wangu.
Huyu bwana alikuwa jirani yangu na ofisa mkubwa katika serikali tukapendana sana na kwake nilikuwa sipungui.
Mzungumzaji wangu na "intellect," yake kali sana na mtu wa dini.
Mtu mwema yeye na familia yake.
Wanae wana akili si mchezo Mashaallah.
Siku moja katika mazungumzo akaniambia kuwa yeye alishiriki katika mapinduzi na alibeba bunduki.
Nilishtuka kwa kuwa najua nini maana ya kubeba bunduki katika mapinduzi.
Miaka ikapita nami nimesahau historia ile hadi iliponijia ghafla kama ilivyonifikia.
Katika miaka ya hivi karibuni iko siku nilikwenda kumtembelea sahib wa sahib na akafurahi sana kuniona nimetia mguu nyumbani kwake.
Kwa kuwa alikuwa anafahamu mapenzi yangu katika historia akanichukua hadi kwenye ukuta ambapo alikuwa ametundika picha zake za mapinduzi.
Akanionyesha picha moja wako vijana watatu wamevaa unifomu za jeshi na wote wamebeba silaha akaanza kunitajia majina kwanza yeye mwenyewe kisha mwingine na akamalizia a jina la rafiki yangu aliyenieleza kuwa alishiriki katika mapinduzi na alibeba bunduki.
Waingereza wana msemo, "Seeing is believing."
Nilimfahamisha mwenyeji wangu kuwa tunafahamiana miaka mingi na tulikuwa majirani.
Katika kitabu hiki historia mfano wa haya ninayoeleza hapa ziko nyingi.
Wapinduzi wanazo kumbukumbu na wanazionyesha na kuyahadithia yale yaliyopitika Zanzibar.
Historia ya mapinduzi ya mwaka wa 1964 ni historia ambayo wapo wanayoionea aibu na wako ambao wana ujasiri wa kuieleza na kile walichofanya kuiangusha serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.
Si kila siku tutakutana na Baraka Shamte au Biubwa Amour Zahoro.
Lakini Wapinduzi wanapozungumza ni vyema tukawasikiliza kwani yapo mengi ya kujifunza kutoka kwao.