mzizi mkavu mbona upo agresive hivyo hiyo sio tabia ya kitabibu kaka.
Na sijasema umekosea nimesema kama ana 35 ushauri wako hauto msaidia maana umefanya mahesabu kutumia 28 days. Lakin naona siku zako ni 28 days so ushauri wa mzizi ni muhimu.
Anyaway dada angu nikusaidie ili siku nyingine usisumbuke kuuliza tena
na inaoneka mzunguko wako ni 28 days
1. Kawaida kama ni 28 days
ovulation ni siku ya 14 then toa siku mbili, na unaongeza siku mbili. Maana yake siku za kupata mimba ni siku ya 12-16 kumbuka siku ya kwanza kuesabu iwe first day menses.
2. Kama una mzunguko 21 days siku za kupata mimba ni siku ya 5-9
3. Na kama una mzunguko wa siku 35 siku za kupata mimba ni siku ya 19-23
kumbuka siku ya kwanza kuhesabu iwe siku ya kwanza ya damu.
Lakin wewe tumia option 1