Mwanamke,Simu na Ugomvi

Mwanamke,Simu na Ugomvi

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Sio siri tena ni dhahiri kuwa mwanamke hutumia sim au hushika sim mara nyingi kuliko mwanaume

Matumizi ya sim kwa mwanamke yamekuwa ya hali ya juu na imekuwa ni njia sasa ya kuwasilisha shida au kero yake kwa mwenzi/mume/ ndugu,jamaa na marafiki

Bahati mbaya ni kuwa wanawake wengi kwa sasa wanatumia njia ya sim kulalamikia mpenzi/mume wake pale anapokerwa na jambo fulani ambalo amelisikia , ameambiwa kutoka kwa mtu ,au ameliona yeye mwenyewe

Siku hizi mwanamke akimuona mume/mpenzi amefanya kitu kinachoashiria kumsaliti hawezi kukuita uso kwa uso mkaaa akaanza kukuuliza kuhusu aliyoyaona au aliyoyasikia

Badala yake hukaa na kuandika SMS ndefu hasa kwa kutumia WhatsApp ambamo hakuna ukomo wa urefu wa SMS na kutitiririka kuhusu mwanaume

Hata kama mmeshinda pamoja usiku kucha au mchana kutwaa ,hata kama wakati mmelala kuna namba ngeni yenye utata ilikuwa inapigwa kwenye sim ya mwanaume hawezi akahoji badala yake atasubiri kukuche na pale utakapoondoka kutoka mazingira yake utakutana na bonge la SMS lenye page zaidi ya kumi akilalamika

Na pia siku hizi wanawake wanatumia simu sana hasa SMS kuomba matumizi

Mfano,mnaweza mkawa pamoja akawa na shida na hela,baada ya kuondoka dakika 5 akakutumia sms ya kuomba hela sijui umtumie kwa mpesa sijui cha msingi ameomba hela

Athari zake

Mwanamke unapotumia sim kuwasilisha malalamiko yako kwa mume au mpenzi na huku kuna uwezekano wa kuitana na mkaongea uso kwa uso ni hatari zaidi katika mahusiano

Uso wa mwanamke una nguvu sana pale anapoeleza shida yake mbele ya mwenzi wake,sura ya mwanamke humfanya mwanaume ashuke na afikirie mara mbilimbili kuhusu malalamiko yako na pia hupunguza ule ukali wa kurushiana maneno machafu kuliko kutumia sim ambapo hujikuta mnarushiana makombora ya matusi na kejeli na hatimaye SMS ya mwisho huweza kuandikwa "Mimi na wewe basi"

Asanteni
 
Jamani uso umeumbwa na haya, halaf me niko mitondooni huku babe yuko mabwepande had tukikutana ni mda kidogo bado tu nisubiri tukutane ndio nimwambie makosa yake??

Ntakuambia hapo hapo kama tuko pamoja ntakuface kama tuko hivi mbali sim itahusika siwezi kulala nasononeka moyo kumbe uwezo wa kukwambia ninao
 
Jamani uso umeumbwa na haya, halaf me niko mitondooni huku babe yuko mabwepande had tukikutana ni mda kidogo bado tu nisubiri tukutane ndio nimwambie makosa yake??

Ntakuambia hapo hapo kama tuko pamoja ntakuface kama tuko hivi mbali sim itahusika siwezi kulala nasononeka moyo kumbe uwezo wa kukwambia ninao
Kama kuna uwezekano wa kumwambia uso kwa uso bora tu umwambie kuliko kusubiri muachane ndo uanze kutiririka kwenye meseji
 
Back
Top Bottom