Mwanamke sio rafiki Frank na Nesto wapo kanisani

Mwanamke sio rafiki Frank na Nesto wapo kanisani

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
C&P
Frank: Nesto Kwa Nini Mwanamke Yule Ananitazama Hivi?

Nesto:mwanamke Yupi?

Frank:yule Pale Kavaa Gauni Ya Bluu.

Nestor:usimtazame Kamwe achana nae.

Baada Ya Dakika Chache Frank Akasema Tena lakini Nesto Anani Konyezea Jicho!
Nesto: nimeshakwambia Usimtizame wewe sikiliza mahubiri.

Baada Ya Misa Frank Akapotea Na Nesto Akaja Kumuona Saa 5 Usiku.

Nesto: frank Ulipitia Wapi Tangu Mchana Saa 6 Mpaka Hivi?

Frank: Ndugu yangu Ni Story Ndefu Nimechoka sana hapa nilipo,yaani niko hoi!!!
Nesto: story Ndefu Kulikoni?

Frank: tulipotoka Kanisani Yule Mwanamke Akaniita Tukaongea vizuri tu halafu Tukaenda Kwake Tukala chakula Ila Alipotaka Kunikumbatia Tu Mumewe Askari Akaja Yule Mama Akasema Mumewe Ni Mkali Sana Ataniua Kwa Hiyo Akanipa Nguo Nyingi Sana Zilizo Kuwa Kabatini Nikajifanya Mpiga Pasi Nguo.

Nesto: yaan Toka Mchana Mpaka Hivi Saa 5 Usiku umekuwa unapiga Pasi Tu?

Frank: Ndio Kaka,na vyombo juu nimeosha na kusugua masufuria.

Nestor: Nilikwambia Usimuangalie Hukusikia Unatakiwa unisikilize ninapo Kwambia Kitu.

Unaona Zile Nguo Ulizo Piga Pasi Mimi Ndio Nilizifua Jumapili Iliyopita.

Na Mimi Kanifanyia Hivyo Hivyo Kaka na nimeambiwa ni mpango wao na mumewe ndio maana hawaajiri wafanyakazi wa ndani.

#Copied
 
Back
Top Bottom