Mwanamke usimdanganye mumeo hujazaa!

Huyo jamaa amesusa msiba lakini ajue tatizo la kutokua na mtoto ni la kwake si la mkewe.
Kazi kwake sasa aende akapime kwa daktari
 
rekebisha kichwa cha habari tafadhali....
wanaodanganya na kuficha watoto ni wanaume na wanawake sio wanawake pekee....
 

hili tatizo siyo la wanawake tu. sisi watanzania tulio wengi hatuwezi kusema ukweli, iwe wanawake au wanaume. pale tunapoona tunapapenda, wengi wetu tunapoteza uwezo wa kusema ukweli, tukifikiri kuwa tutakataliwa.hatuwezi kuacha kusema uongo kwakuwa hatujajaribu ukweli na kupata faida yake. wengi wetu ni wa ongo ktk nyanja zote.

chukua mfano, uingie ktk matatizo na mtanzania wa leo, say amepotelewa na kitu ktk mazingira wewe ulikuwapo. uwe umeiba au hujaiba, atakapo tangaza kupotelewa lazima ataongeza idadi au thamani ya vilivyo potea, atatia na chumvi ya maneno mengine mengi. matokeo yake hata pale tunapo peleka kesi mahakamani zile chumvi na uongo, zina gundulika na hata kufanya ule ukweli wa msingi kupotezwa na uongo.

tazama chumvi za kamanda kova,pccb ktk kesi ya muro

kwetu sote;
tujifunze kusema ukweli, ukweli unafaida kuliko uongo. ukweli unaleta kujiamini, na ukimkamata mtu ukamshawishi kwa kusema ukweli , hata upendo wake unakuwa ni usio na mashaka
 
Mi staki kujua hayo ya zamani.Kama alikuwa na mtoto au anao..sihitaji kujua.
Akinifica so much the better.Mradi ahudumie mwanae kimyakimya bila kunihusisha.
 
ni makabila gani yanaongoza kwa kuficha ukweli? hili ni muhimu kulifahamu ili mtu unapotafuta mchumba ukidondokea kwenye hilo kabila ufanye full check up....nyumbakubwa tufahamishe pls..
Mie nawataja kama wataniua waniue ila ukweli ndio huo..... Wanawake wa kabila la kirangi wengi wana hiyo tabia sana ya kuficha watoto...



Back to topick: ni ulimbukeni wa hali ya juu na naungana na aliyesema kuwa ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi...kama mwanaume kakupenda hata ukimwambia umezaa watoto 10 hawezi kukuacha, kwani kuwa na mtoto/watoto ni dhambi kwenye jamii? Tena basi hakuna dhambi mbaya kama mwanamke mzima na akili zako unabeba mimba miezi 9 kisha unazaa kwa uchungu afu eti unakutana na mtoto wa mwanamke mwenzio unamkana mwanao loooh.... Ni aibu kumtelekeza mtoto kijijini kwa bibi na kumlazimisha akuite shangazi/ dada/ mamdogo n.k..
 
Mbaya sana. Hawajui ukweli unamuweka huru mtu.
 
kumbe warangi ni kiboko...........duh...inatakiwa kuwa mtafiti kabla hujadondokea humo kwenye mahusiano...
 

Tena umesema kweli, kuna bro. mmoja nafanya kazi naye ofisi moja alikuwa na mke wakapata wototo wawili, bahati mbaya mke akafariki mtoto wao wa pili akiwa mdogo sana (1.5yrs). Baadaye akaoa mdada mwingine ambaye alimkuta na kabinti kake. Mkaka aliwatambulisha kwa mke wake huyu wale watoto wawili tu wa marehemu, kumbe mshikaji ana msululu wa watoto kabla ya ndoa yake ya kwanza. Sasa ameshaona yule mke yuko fair kwa wototo aliowakuta ameamua kuleta kundini mtoto mmoja baada ya mwingine na ameshaleta watatu mpaka sasa. Mdada anajiuliza sijui christmas hii atapata mtoto mpya ama la . Na zote ni ndume copy right na baba yao mpaka kuwatoa nduki nomaaaaaa. Kwa hiyo ni yetu sote waume kwa wake.
 
rekebisha kichwa cha habari tafadhali....
wanaodanganya na kuficha watoto ni wanaume na wanawake sio wanawake pekee....

Natamani ungesoma paragrafu ya mwisho pengine usingeweza kupost
 

Nadhani huyu dada alisahau ule usemi usemao "kuwa mkweli leo ili usiadhirike kesho" angekuwa mkweli tangia mwanzo yote hayo yasingetokea sasa wana Jf tujifunze kwa kosa la mwenzetu huyu kuliko kuja kujifunzia kwenye makosa yetu wenyewe
 

Tuwekane wazi ni kabila gani hilo?
 

Mimi simoooooooooooo! mwenyewe niliileta thread bila kutaja kabila hapa. Tena una bahati wahusika wamekaa kimyaaaaaaa, ingekuwa wale jamaa wa midizini, ndo ungejua leo nini kilisabababisha tumbusi akose manyoya shingoni. Narudia mie simoo, na naomba thread hi isichafuliwe kwa kutajana kabila jamani, wenyewe hawapendiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, ooooooooooh!
 
Hivi mtu anakudanganya kuwa alikua na mtoto unakuja kugundua unakasirika vibaya,tatizo linakua hasa wapi?Uongo uliolishwa au ni mtoto uliekua hata humlei?Au ni mazoea?
 
Hivi mtu anakudanganya kuwa alikua na mtoto unakuja kugundua unakasirika vibaya,tatizo linakua hasa wapi?Uongo uliolishwa au ni mtoto uliekua hata humlei?Au ni mazoea?
Uongo ndio tatizo. . . wengi hawajali kulea/ matumizi wanajali kutokuambiwa ukweli.
 
Hakuna mtu anayempenda mtu muongo,leave aside awe ndo mwenza wako wa maisha. Maana utajiuliza mengi sana mfano ni mangapi mengine aloficha.

Hivi mtu anakudanganya kuwa alikua na mtoto unakuja kugundua unakasirika vibaya,tatizo linakua hasa wapi?Uongo uliolishwa au ni mtoto uliekua hata humlei?Au ni mazoea?
 
Afu mi naona watoto waliokuwa kind of rejected na wazazi wao huwa wanakuwa na tabia tofauti kidogo.
1. defensive nature, hujamguza lakini atakavyokuja na ushahidi kwamba hakufanya yeye kosa ni mkubwa kweli
2. Kutojiamini, mkiwa naye anahisi mnamchukia hata kama hakuna haja ya kuhisi hivyo
3. trust, haamini mtu hata mmoja ile ya kiukweli siku zote yko kimachale machale tu haamini mtu hata mmoja
4. Love, hata unconditional affection kwa mtu hata. Anampenda mtu foa a reason labda anapata kitu fulani toka kwake na aina hizo. Lakini kumpenda mtu freely ngumu sana kwao
5. Kisasi, du bahati mbaya umeingia kwenye kumi na nane yake kisasi chao huwa ni kikali kweli. Wanaishi by jino kwa jino rule.

Basi mie huwa napata shida kuwa nao katika mtiririko wa kila siku wa maisha maana wako siwezi hata elezea hadi ukae nae ndo labda mtanielewa hapa.
 
Wana JF mimi nipo tofauti na hili swala la kuhusisha makabila ya watu na hii tabia ya kuficha watoto wa ujanani. MSIMAMO WANGU NI HUU TABIA HII IPO KARIBU KILA KABILA NA INATOKANA NA MAKUZI YA FAMILIA HUSIKA NA SI KABILA

Mchango wangu kwa topic hii ni Wazazi na walezi wawafundishe watoto wawe wa kike au wa kiume KUWA WAKWELI na kwa kuwa wakweli ndipo jamii itaondokana na tabia mbalimbali zisizofaa km hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…