Mwanamke wa kwanza kuwa Gavana, ndie huenda pia akawa mwanamke wa kwanza kuwa Naibu wa Rais Kenya, atakuwa wa tatu Afrika Mashariki

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Anne Mumbi Waiguru, Govonor wa Kirinyaga ana nafasi kubwa mno ya kuteuliwa kua Naibu wa Rais Kenya, baada ya Rigadhi Gachagua kubanduliwa.

Swali ni je,
Rais, Dr. William Ruto atatimiza ahadi yake ya kuwa na usawa wa kijinsia uongozini, kuanzia ngazi za juu kwenye chama na serikali, mapema zaidi kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2027?

Uwezekano huo mkubwa unajiri kulingana na ahadi ya Rais Dr. William Ruto aliyoitoa March 07.2024, katika Baraza kuu la magavana wanawake nchini Kenya, na kusisitiza kwamba ataendelea kujitolea kuhakikisha kuwa sheria ya thuluthi mbili ya jinsia imetekelezwa kikamilifu katika chama chake cha United Democratic Alliance (UDA) na katika serikali ya Kenya Kwanza kwa jumla.

Wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Baraza la Magavana Wanawake G7 jijini Nairobi mwezi March mwaka huu 2024, Dr. Ruto alisema kuwa serikali yake imefuata mikakati mikali ili kutimiza kiwango cha ujumuishaji wa kijinsia katika katiba na atakuwa mstari wa mbele kuonyesha kwa mfano alichosema.

“Wakati Riggy G (Naibu rais Rigathi Gachagua) na mimi tukikubaliana jinsi mambo yatakavyokuwa siku za usoni lazima pia tukubaliane kwamba kwenda mbele ikiwa mwanamume ni mgombea wa urais, mwanamke lazima awe mgombea mwenza, na ikiwa mwanamke ni mgombea, mwanamume anafaa kuwa mgombea mwenza," Ruto alisema katikati ya umati wa watu waliokuwa wakishangilia.

Aliongeza: "Lazima tufanye kwa kukusudia kuhusu hilo vinginevyo halitatokea kamwe."

Ruto alisema kuwa hayo pia yanafaa kufanywa kuwa ya lazima kwa Magavana na nyadhifa zote za uongozi ndani ya chama.

Alionyesha imani kuwa viongozi wengine wa chama cha UDA, watapokea vyema pendekezo la kufanikisha kikamilifu kanuni ya thuluthi mbili ya jinsia kikatiba.

JE,
Dr.Ruto anaweza kutimiza ahadi yake hii mapema zaidi ya 2027, ambayo ni fursa kwa wanawake wa Kenya na Africa Mashariki?

Anne Waiguru ni Govonor wa kwanza mwanamke Kenya. Je, anaweza kua naibu wa Rais mwanamke wa kwanza Kenya?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mke Mdogo wa Mstaafu mla ganja. Kenya wanachezeshewa mchezo WA karata 3 bila kujua. Kibera/Gen Z mtasubiri sana
 
Back
Top Bottom