Habari za wakati huu wakuu
Mwanamke wangu nilieishi nae kwa miaka mitatu anenifanyia jambo la kikatili sana katika maisha yangu, ni mwanamke pekee niliempeleka nyumbani kwetu kumtambulisha
Hatimae siku ya jana nimeweza kujua ukweli kuwa amenisaliti
Nilimuaga kuwa nasafiri kikazi nitakaa week mbili mkoani lakini matokea yake nilikaaa week moja tu
Wakati narudi mkoani nilifika nyumbani na kumkuta hayupo nikawaulizia majirani na kuniambia huyu mtu hayupo yapata week sasa na aliwaambia anaenda kwao kusalimia
Na mimi nikampigia simu kumuuliza yuko wapi, akaniambia yuko nyumbani nikamwambia mbona mm niko nyumbani toka jana na sijamuona, nikamwambia arudi nyumbani haraka sana kweli baada ya kupita lisaa limoja akarudi nyumbani
Nikamuuliza ulikuwa wapi week nzima na hukuwa nyumbani, akaniambia nilikuwa kwa rafiki yangu niliona kukaa pekee yangu nitakuwa mpweke, nikamuuliza wakati unaondoka kwanini hukunipa taarifa yoyote, nikachukuwa simu na kumpigia rafiki yake aliesema yupo kwake, maajabu rafiki yake alikataa kuwa huyo mtu hakuwa kwake hata siku moja
Nikaanza kumpiga huku nikimwambia aseme kweli alikuwa wapi,akawa anahapia kuwa alikuwa kwa huyo huyo rafiki yake ambae kamkataa, nikachukua simu yake na kufanya upekuzi ndipo nilipobaini namba ya simu ambayo imefutwa na ilikuwa imesaviwa Mine♥️, hapo ndipo alipoanza kutetemeka na kulia huku akisema kuwa huyo jamaa amekuwa akimtongoza mara mara na kumkataa huku akiwa analia na kuapia kwa jina la mungu, wakati huo na kipigo kinaendelea
Nikaamua kuipiga ile namba kwa kutumia simu yake, jamaa alipokea na kumuita mke wangu, roho iliniuma sana, jamaa nikamwambia mimi kaka yake huyu bint kapata matatizo, jamaa akasema sawa nakuja hapo fasta, nilishaangaa kuwa jamaa anapajua mpaka ninapokaa
Alivyofika nikamwambia huyu ni mwanamke wangu wa muda mrefu, na ansema alikuwa kwako je ni kweli, jamaa akaniambia kweli alikuwa kwangu kwa muda week nzima, nilijiskia vibaya mpaka nguvu ziliniisha mwilini nakukaaa chini,
Nikamuuliza mwanamke wangu je ni kweli ulikuwa kwa huyu jamaa, mwanamke wangu akaniambia ni kweli nilikuwa kwake 🥺 mwanamke niliemtarajia kufunga nae pingu za maisha kaamua kunisaliti, nikamuuliza sababu ni zipi zilizofanya unisaliti akaniambia mbele ya jamaa kuwa simuhudumii vizuri kuna vitu huwa simpi kama akitaka nguo mpya ni hicho tu
Nikamwambia kweli mke wangu umri wote huo unawaza kuvaa na kupendaza na wala sio kufanya maisha yatakayofanya tuishi vizuri hapo baadae na nikamwambia hata kama ulikuwa unataka nguo ulikuwa unashindwa kuniambia mume wangu kuna nguo nimeipenda nataka uninunulie je nisingekuoa pesa, oooh sasa kila kitu mpaka nikuambie kiukweli nilikosa nguvu sana,
ukweli nikwamba huyu mwanamke kanizidi miaka mitano ki umri, nilikuwa natarajia kuwa mwenzangu kanizidi umri basi atakuwa mtu sasa kwangu kwa kujua kuwa ameshamaliza mambo ya ujana sasa tufanye maisha lakini kumbe nimegundua bado hajamaliza mambo yake na pengine hata huko nyuma alikuwa akinisaliti sana bila ya mimi kujua, hatimae jana nimeweza kujua kuwa sio mwanamke sahihi kwangu
Usiku wa kuamkia leo usingizi wangu ulikuwa taabu sana huku nikimuangalia nimfanye nini huyu mwanamke kwanini kaamua kunifedhehesha sana naweka wapi uso wangu nikitembea huko barabarani, ndugu zangu nipo katika hali ngumu sana ya kimawazo.