Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Wanaume wengi wafujaji au watesaji wa wake zao hujitahidi sana kumtenganisha mke na ndugu zake. Wanapofanikiwa kuwatenganisha, wanaume hao huwa wamejitengenezea wigo mpana zaidi wa kuwadhibiti wake zao. Kama mjuavyo lengo la ufujaji kwenye ndoa ni kudhibiti. Mwanaume anapomkosanisha mkewe na ndugu zake anakuwa na uhakika kwamba, mke huyo hana nafasi ya kuondoka kwake kwa sababu hana pa kwenda.
Lakini kwa kumgombanisha na ndugu zake, mwanaume anapata nguvu ya kumfanya mkewe ahisi kushtakiwa na dhamirana kuanza kuhisi kwamba, ni yeye mwenye matatizo na siyo mumewe, kwani hata ndugu ameshindana nao. Mume pia humkumbushia kwamba ameshindwa hata kuelewana na ndugu zake, yeye ataweza wapi. ‘Ndugu zako tu wamekushindwa , mimi nitaweza wapi?' anaweza kusema hivyo.
Kwa mwanaume mfujaji, kumgombanisha mkewe na ndugu zake ni jambo la kawaida sana na hufanywa kwa sura mbalimbali. Kwa mfano, mume anaweza kuwaambia ndugu wa mke kwamba mkewe amebadilika sana kwani amekuwa ni mchoyo na hapendi wageni. Na ili kujenga mazingira ya kuthibitisha hilo anaweza kumkataza mkewe kuwahudumia ndugu zake kwa kinywaji chochote wanapokuja nyumbani kuwatembelea. Kwa hiyo ndugu wanapofika hapo nyumbani wakati mume akiwepo, mume huyo kusubiri hadi kiasi cha nusu saa halafu humwambia mkewe, ‘vipi, wageni hawanywi hata soda?' hapo mkewe atawaletea wageni soda, na wageni hao watakuwa wamethibitisha yale maneno waliyoambiwa na mume wake.
Njia nyingine ni ile ya mume kusaidia sana ndugu wa mke lakini wakati huo huo akitia sumu mbaya dhidi ya mkewe. Anaweza kumpa fedha shemeji au hata baba au mama mkwe na kusema, 'lakini mwenzangu asijue kwa sababu kidogo mambo ya kusaidia hayapendi sana, lakini msimwambie.'
Nyingine ni ile ya kuwaambia ndugu mambo mabaya dhidi yao ambayo mkewe alimwambia katika mazungumzo ya kutaka aijue familia yake vizuri. ‘Sasa hayo mambo ya kifamilia mimi ningeyajua vipi?' mwanaume atahoji, na itakuwa ni kweli.
Kuna njia ya kumwambia mke kuhusu ubaya wa ndugu zake. Anaweza kusema kwamba, dada wa mkewe amemwambia kwamba, zamani huyo mkewe alikuwa muhuni . ‘huna haja ya kumuuliza, kaa naye mbali tu, mwepuke huna haja ya kumpa msaada mtu kama huyo. Amenikera sana.' Anaweza kumuonya mkewe. Kwa sababu mke anamwamini mume na hataki mume huyo akasutana na dada yake, hunyamaza tu. Lakini hujenga chuki dhidi ya dada yake.
Mwanamke anashauriwa kuwa mwangalifu sana na mwanaume mfujaji, hasa linapokuja suala la kumgombanisha na ndugu zake. Kama mume akimwambia mkewe mambo mabaya kuhusu ndugu wa mke huyo, inabidi uchunguzi ufanyike. Mwanamke hapaswi kuamini kila kitu anachoambiwa na mumewe kuhusu ndugu zake……………………………