Mwanamme ajiua baada ya kufumaniwa akitongoza binti wa kidato cha kwanza

Mwanamme ajiua baada ya kufumaniwa akitongoza binti wa kidato cha kwanza

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
John Mhagama (42) mkazi wa mtaa wa kanisa B, wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe amejiua kwa kunywa sumu baada ya kufumaniwa na mke wake akiwa kwenye mazungumzo ya kimapenzi na binti wa kidato cha kwanza anayeishi nyumba jirani na yao.

Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na tabia ya kwenda kununua mkaa kwa jirani kila ifikapo jioni, kumbe alipokuwa akienda huko anakutana na binti huyo na kumpa pesa.

Akizungumzia tukio hilo jana Jumatatu, Septemba 12, 2022, Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo alipozungumza na waandishi wa habari.

“Siku ya tukio marehemu alikwenda kununua mkaa kama kawaida yake, lakini siku hiyo mkewe alikuwa akimfuatulia kwa nyuma na kumuona akiongea na binti na kumpa Sh5,000 huku akimbembeleza kumkubalia ombi lake la mapenzi, kwani amekuwa akichukua pesa zake pasipo kumtimizia,” amesema.

Alisema baada ya mkewe kuwaona alijitokeza na kuanza kumlaumu mumewe kwa kitendo alichofanya, lakini kwa hasira mumewe huyo alimpiga mkewe na kisha kwenda kusokojulikana.

Aliendelea kusema kuwa, baada ya mkewe kuhojiwa na Polisi, alisema mumewe hakurejea nyumbani na ndipo baadaye alipigiwa simu na shangazi wa marehemu akimjulisha kuwa mumewe huyo ana hali mbaya, hivyo alipokwenda kumpeleka hospitali ambako alipoteza maisha.

Kamanda Issa aliitaka jamii kutokuwa na wivu ulio pitiliza kwani mara nyingi matokeo yake huwa mabaya na kupelekea vifo.

Mwananchi
 
𝐇𝐚𝐩𝐨 𝐚𝐧𝐚𝐥𝐚𝐮𝐦𝐢𝐰𝐚 𝐚𝐥𝐢𝐞𝐣𝐢𝐮𝐚 𝐥𝐚𝐛𝐝𝐚 𝐚𝐥𝐢𝐤𝐮𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐧𝐲𝐢𝐦𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐤𝐞𝐰𝐞 𝐣𝐞[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kamanda Issa aliitaka jamii kutokuwa na wivu ulio pitiliza kwani mara nyingi matokeo yake huwa mabaya na kupelekea vifo."

Hili ni hitimisho la kipuuzi mno kutolewa na kamanda,angeacha kila mtu atafakari kivyake tu

Kwani kosa la mke hapo ni lipi?kwanza alikuwa anamuoka na miaka 30 mmewe,pili kaokoa mtoto kubakwa,tatu alikuwa anaokoa ndoa yake,hayo ni ya kumshukuru mno,mume kajitakia mwenyewe
 
Akili za akina John wanazijua wenyewe. Huyu anahonga elfu 5 kila siku, yule mwingine alikuwa anahonga nyumba za serikali na ukuu wa wilaya. Ukiwa mzuri kama Angela au ummy unapewa ucabinet kabisa.

R.I.P Faru John!
 
Jamaa itakuwa alikuwa na stress tu nyingine pia
 
Kufumaniwa tu anatongoza anajiua angefumiwa wapo kitandani
 
Njombe na Geita ni too much sasa

Halafu mzee anatongozaje kiboya . ..kila siku unakapa elfu tano
 
Back
Top Bottom