TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
PICHANI: Binti mdogo Mona aliyekuwa mke wa muuaji aitwaye Sajjad Heydari.
Katika hali ya kusikitisha, kijana mmoja nchini Irani amemchinja pichani juu binti aliyekuwa mkewe kutokana na kumkimbia kwa sababu mateso na manyanyaso ndani ya Ndoa yao.
Binti huyo mdogo aliolewa akiwa na miaka 12 na alibahatika kupata mtoto wa kiume alipofikisha miaka 14, bahati mbaya Ndoa yao ilianza misukosuko na Sajjad akiwa anampa kipigo binti huyo.
VIDEO: Ikimuonyesha kijana Sajjad akitembea na kichwa cha aliyekuwa mkewe mtaa huku kabeba panga.
Habari kutoka mahakamani zinadai kuwa kutokana na hali ya kutoelewana ndani ya ndoa hiyo binti huyo alikuwa akidai talaka ila mumewe aligoma kutoa na ndipo alifanya uhamuzi wa kutoroka.
Alikimbilia nchini Uturuki kuepusha ukatili aliokuwa akifanyiwa, ila baadaye familia yake ilimhakikishia usalama endapo angerejea nchini kwao.
Kutokana na kosa hilo mahakama ilitoa hukumu ya miaka 8 kwa sababu familia ya marehemu ilimsamehe muuaji na kwa sababu baba wa Mona hakutoa baraka ili binti yake achinjwe!.