Mwanamuziki Dj Arafat afariki baada ya kugongwa na gari

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Arafat-Dar24.jpg

Ange Di Huon maarufu kama DJ Arafat, msanii maarufu kutoka Ivory Coast amefariki dunia leo, Agosti 12, 2019 baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia leo.

Mfalme huyo wa ‘coupe decale’ amepoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitalini mjini Abidjan, kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha kugongwa na gari, kwa mujibu wa Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo, Maurice Bandaman.

Waziri Bandaman amesema pikipiki aliyokuwa anaiendesha Dj Arafat iligongwa na gari lililokuwa linaendeshwa na mtangazaji maarufu wa redio nchini humo.

Daktari wa hospitali aliyokuwa anapatiwa matibabu amewaambia waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa jina kuwa msanii huyo alikuwa amepasuka sehemu ya fuvu.

“Alilazwa kwenye chumba cha dharura akiwa kwenye hali mbaya. Alikuwa na jeraha/mpasuko kwenye eneo la fuvu. Tulijaribu kumsaidia na kuokoa maisha yake lakini tulishindwa” daktari aliwaambia waandishi wa habari.
Taarifa za kifo cha Dj Arafat zilitolewa na Waziri wa Utamaduni, Bandaman.

“Niko hospitalini muda huu alipokuwa amelazwa DJ Arafat na naweza kuthibitisha kuwa amefariki dunia,” Bandaman anakaririwa na Jeune Afrique.

Wimbo wa mwisho alioutoa ni ‘Moto moto’ ambao hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 4.4 kwenye YouTube ndani ya miezi mitatu.
 
Kuna kideo cha CCTV Instagram yeye ndio aligonga gari, alikuwa spidi sana kuendesha pikipiki kwa kuinyanyua kama kawaida yake.. hakuona gari ilishaingia barabara aliyokuwepo akitokea mbali.. na dereva hakuwa na kosa akaigonga kwa nyuma alipokuwa anashusha pikipiki chini na bang akaanguka
R.I.P
 
"Aliyemgonga ni mtangazaji wa radio maarufu mjini humo"...

Mmh !! Haya!! [emoji102]
 
Innalillah wainnailillah raijuun, ila sijui kwanini taarifa nyingi za miss Zomboko ni huzuni
 
Kuna kideo cha CCTV Instagram yeye ndio aligonga gari, alikuwa spidi sana kuendesha pikipiki kwa kuinyanyua kama kawaida yake.. hakuona gari ilishaingia barabara aliyokuwepo akitokea mbali.. na dereva hakuwa na kosa akaigonga kwa nyuma alipokuwa anashusha pikipiki chini na bang akaanguka
R.I.P
weka kavideo tujionee mkuu
 
Arafat-Dar24.jpg

Ange Di Huon maarufu kama DJ Arafat, msanii maarufu kutoka Ivory Coast amefariki dunia leo, Agosti 12, 2019 baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia leo.

Mfalme huyo wa ‘coupe decale’ amepoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitalini mjini Abidjan, kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha kugongwa na gari, kwa mujibu wa Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo, Maurice Bandaman.

Waziri Bandaman amesema pikipiki aliyokuwa anaiendesha Dj Arafat iligongwa na gari lililokuwa linaendeshwa na mtangazaji maarufu wa redio nchini humo.

Daktari wa hospitali aliyokuwa anapatiwa matibabu amewaambia waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa jina kuwa msanii huyo alikuwa amepasuka sehemu ya fuvu.

“Alilazwa kwenye chumba cha dharura akiwa kwenye hali mbaya. Alikuwa na jeraha/mpasuko kwenye eneo la fuvu. Tulijaribu kumsaidia na kuokoa maisha yake lakini tulishindwa” daktari aliwaambia waandishi wa habari.
Taarifa za kifo cha Dj Arafat zilitolewa na Waziri wa Utamaduni, Bandaman.

“Niko hospitalini muda huu alipokuwa amelazwa DJ Arafat na naweza kuthibitisha kuwa amefariki dunia,” Bandaman anakaririwa na Jeune Afrique.

Wimbo wa mwisho alioutoa ni ‘Moto moto’ ambao hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 4.4 kwenye YouTube ndani ya miezi mitatu.
Miss zomboko katika ubora wake
 
Back
Top Bottom