TANZIA Mwanamuziki mkongwe Ismail Issa Michuzi amefariki leo akiwa Muhimbili

TANZIA Mwanamuziki mkongwe Ismail Issa Michuzi amefariki leo akiwa Muhimbili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanamuziki mkongwe Ismail Issa Michuzi amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.

Ismail, ambaye ni kaka yake mpiga picha maarufu na blogger Muhidin Issa Michuzi, amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Ismail atakumbukwa kuwa mmoja wa viongozi na waanzilishi wa bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho.

Baada ya Dar International kudumaa Ismail alijiunga na Jeshi na kuingizwa katika bendi ya Mwenge Jazz kama mpuliza trumpet.

Alitumikia jeshi hadi alipostaafu takriban miaka sita iliyopita na kuhamia Tukuyu Mbeya ambako alifanya kazi kwa Muda na Radio Chai FM.

Mipango ya mazishi inafanyika Tabata Mawenzi, Dar. Taarifa kamili za maziko baadae

1622714028360.png
 
Poleni wana familia, Mungu na awe mfariji wenu kwa kipindi hiki kigumu.
 
Pole kwa familia, Bwana awafariji kwa msiba huu

Hebu toa direction vizuri mkuu ni mawenzi sehemu gani jioni nipunguze bajeti ya menu maana nitakuwa kimanga
 
Rest in Peace Mwendazake
Nilikuwa najua eti "MWENDAZAKE" ni mmoja tu! Kumbe nilikuwa wrong!
…….. Mwenye Enzi Mungu ampumzishe pahala pema!! Pia, awape moyo wa uvumilivu na faraja ndugu na jamaa zake!
 
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie. Apumzike kwa Amani
 
Mwimbo upi maarufu aliimba,au zlikua bendi gani?
R.I.P mzee wetu.
 
Serikali iliyopita tungesikia matatizo ya mfumo wa upumuaji
 
Back
Top Bottom