Nadhani ushauri wako ataupokea. Unashauri afanye nini ili afike kwenye hivyo vinamiss kwake??
Binafsi, nakubaliana na mchangiaji mmoja hapo juu, huyu binti angekuwa mbele ingekuwa habari ingine.
Sure angekuwa habari nyingine ila hata hapa akiamua anaweza kuwa habari nyingine pia. Mungu aliyefanya awe hapa anakusudio lake na nzuri zaidi ameweza kujua anakipaji gani.
Kuhusu nini afanye? Hili swali nitalijibu kwa ujumla. Aina ya muziki anaofanya kama sitakuwa nje ya mstari na mawazo yake ni muziki aina ya Hiphop
Mara nyingi aina ya Muziki huu ili uwe bora zaidi unahitaji utunzi wa "mistari inayoishi". Na hapa ndipo utakapo acha legacy yako katika jamii inayokuzunguka.
Mpaka leo tunaona, mfano Mtu kama 2pac bado anaongelewa kwenye fikra za watu na baadhi ya tungo zake zinafanyiwa remix mpaka kesho, si kwamba alikuwa "bora sana" kuliko wengeni katika kurap, ni vile tu aliweza kuandika "mistari inayoishi"
Hapa Tanzania kuna watu walifanya Muziki na wakapendwa sana na kulipwa pesa nyingi, vile waliweza kuandika "Kuku kapanda baiskeli", ila leo huo muziki ukichezwa tena sijui kama utaweza kukusanya kijiji kama hapo mwanzo.
Tujiulize tena ni kwanini Muziki wa Msondo ukichezwa leo bado unavuta hisia kwa msikilizaji japo unabezwa ni Zilipendwa?
Natumai nitakuwa nimeeleweka kwa kiasi fulani nilichokuwa namaanisha, katika kukosoa kwangu.