Mwananchi ampa Traffic Police Tsh. 500,000 kwa kutekeleza vyema majukumu yake kazini

Mwananchi ampa Traffic Police Tsh. 500,000 kwa kutekeleza vyema majukumu yake kazini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha, Sajenti Anna Kidenge amepongezwa na kupewa fedha Shilingi 500,000 kwa kutoa huduma bora barabarani.

Mwananchi aliyetoa zawadi hiyo amesema ameguswa na namna ambavyo Askari huyo amekuwa akimwona wakati akitekeleza majukumu yake ya usalama barabarani kwa weledi.

Askari huyo alikabidhiwa zawadi hiyo katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili kuwaaga wastaafu pamoja na kuwapongeza askari waliofanya vizuri zaidi Mkoani humo.
 
Duh huwa kuna askari asubuhi na jioni natamani niwape hata 5,000/-. Kuna kazi nzuri sana wanaifanya kuongoza magari.
 
Back
Top Bottom