Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha, Sajenti Anna Kidenge amepongezwa na kupewa fedha Shilingi 500,000 kwa kutoa huduma bora barabarani.
Mwananchi aliyetoa zawadi hiyo amesema ameguswa na namna ambavyo Askari huyo amekuwa akimwona wakati akitekeleza majukumu yake ya usalama barabarani kwa weledi.
Askari huyo alikabidhiwa zawadi hiyo katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili kuwaaga wastaafu pamoja na kuwapongeza askari waliofanya vizuri zaidi Mkoani humo.