Mwananchi: Dr Makaidi na mkewe waondolewe bungeni

theROOM

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
946
Reaction score
419
Uzoefu wetu wa muda mrefu umetuonyesha pasipo shaka kwamba mambo mengi yanayotendeka Tanzania hayawezi kutendeka katika nchi nyingine.

Tanzania imekuwa taifa la ajabu na masikitiko yetu ni kwamba mporomoko wa maadili katika jamii yetu umeziba mitima na dhamira za viongozi wetu na jamii nzima kwa jumla kiasi cha kuyaona matendo hayo kama mambo ya kawaida.

Tunayo mifano ya matukio lukuki ya ajabu na ya kushtusha yaliyowahi kutokea hapa nchini lakini yakaonekana kama ya kawaida.

Fikiria wafanyabiashara walioiba mabilioni ya fedha za Epa ambao muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 walikwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati wa siku za mapumziko na kukwapua mabilioni hayo kwa njia za udanganyifu. Fikiria wezi hao walivyoahidiwa kwamba iwapo wangezirudisha wasingechukuliwa hatua yoyote.

Ebu fikiria nchi ambayo kiongozi wake anakwenda ughaibuni na kutangaza kuwapo kwa majangili mapapa 40 na kusema kiongozi wao yuko mikoa ya Kaskazini, badala ya kusema hayo akiwa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyakamata majangili hayo na kuyachukulia hatua.

Ebu fikiria matukio haya mawili ambapo Waziri Mkuu anatamka bungeni kwamba ni sawa tu kwa Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi ‘wakorofi’, huku mkuu wa nchi akikiagiza chama chake cha siasa ambacho yeye ni mwenyekiti kuwapiga wapinzani anaodai wanafanya vurugu dhidi ya wafuasi wa chama chake. Ni nchi gani ambayo viongozi wake wakuu wanaweza kutoa amri hizo za hatari?

Tumesema yote hayo kutokana na kitendo cha ajabu na aibu kilichofanywa na Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emannuel Makaidi cha kufanya ulaghai na kujiwezesha yeye na mkewe kuteuliwa kuingia katika Bunge la Katiba.

Katika utetezi wake, ametoa hoja za kuchefua na kughadhabisha kuwa, kwa vile mke wake naye ni mwanachama wa chama hicho alikuwa na haki ya kuteuliwa kama ilivyo kwa Rais Kikwete na mke wake ambao wote ni wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

Tunasema uteuzi huo haukubaliki hata kidogo kutokana na kukiuka taratibu zilizowekwa kisheria kwamba vyama vya siasa lazima viwe na sura ya Muungano katika mfumo na uendeshaji wake.

Ni ujasiri na uthubutu wa kiwango cha juu kujiteua yeye na mkewe kama vile NLD ni mali ya kifamilia. Kudai kwamba aliteua majina ya wanachama wanne na Rais akamchagua yeye na mkewe ni uongo wa kupitiliza.

Hii inaonyesha kwamba zilikuwapo mbinu chafu katika mchakato wa uteuzi huo, vinginevyo wanachama wa Zanzibar wangenyimwa vipi uwakilishi? Hatua ya chama hicho upande wa Zanzibar ya kumtaka Rais Kikwete atengue uteuzi wa Dk Makaidi na mkewe lazima iungwe mkono.

Tatizo hapa ni hatua ya Serikali kuendelea kuvibeba kwa sababu za kisiasa vyama vya siasa vilivyokufa siku nyingi. Ukweli ni kwamba NLD na vyama vingine vingi ambavyo kwa mujibu wa sheria ya vyama ya 1992 vinapaswa kufutiwa usajili wa kudumu bado vinatambuliwa kiasi cha viongozi wake kuingizwa katika Bunge Maalumu la Katiba bila kuwa na sifa stahiki.

Source: Gazeti la Mwananchi


My Take:
Hivi usalama wa Taifa hawakufanya vetting jamani kabla ya uteuzi au? Hii nchi haitaisha vituko. Hivi ni kwa nini tunapenda kuwaonea watu wakati taasisi ya Rais anayeteua imefanya makosa ya wazi? Au hatujui Rais ni taasisi na wala sio mtu mmoja. Ingekuwa anafanya kazi yeye peke yake ningemuelewa yaani ajifungie ndani adanganywe, ateue halafu aje aseme walileta majina wao wenyewe..Lakini kwa hili ni lazima mifumo yetu ifanye kazi zake, vinginevyo kuna majanga mengi yatatukuta. Tumesikia eti Kagame anapenyeza watu wake nchini, sijui ni kwa kiwango gani mifumo yetu inayafanyia kazi mambo haya kwa staili hii....
 
Mkuu sio hao 2 kuna huyu mwenyekiti wa udp taifa kamuchukua mdogo wake kuwa mjumbe wa bunge la katiba
 
Huko zanzibar Mwentekiti wa ADC amejichagua mwenyewe chama kibaitisha kikao cha kunfukuza uwanachama.
 
Tutaendelea kulalamika mitandaoni bila kuchukua hatua hadi lini?
Nimesikia BBC mama wa kijana mmoja aliyepoteza maisha katika mgogoro wa Ukraine, anesema yule kijana japo amekufa lakini hakuipenda kabisa serikali iliyopinduliwa (ambayo baadae tunagundua kuwa ilikithiri kwa ufisadi). Na huyo mama anasikitika kupoteza mwanae lakini haonekani kujuta maana anasema amefia kile alichokiamini na yuko listed kwenye 'wakombozi'. Imenigusa sana na bado natafakari uelewa wa hawa watu ukoje ukilinganisha na sisi!

 
Tatizo ni msajili wa vyama vya kisiasa,anatakiwa avifute vyama vyote visivyo na sura ya kitaifa,visivyofanya chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini adi taifa,vinavyoendeshwa kifamilia
 
Muda mwingine nawapenda sana watu wasiokuwa aibu maana mafanikio kwao yanaweza kuja haraka sana........kwa jinsi hili suala lilivyosemwa kama ningekuwa mimi ningeshajitoa au kumwambia wife kaa pembeni..........kwanza kwa kuogopa maneno na kuheshimu sheria za huo ujumbe hata nisingethubutu kupeleka jina la mwenzangu kwa Mh.Rais, lakini huyo Dr....kha! kazi kwelikweli.
 
Kama kawaida uhuni wa posho kumbe wengine wameenda kulelea familia bungeni ndo mana wanataka posho iongezwe
 
Tutaendelea kulalamika mitandaoni bila kuchukua hatua hadi lini?

Makubwa haya.

Kwenye mtandao huwezi kulalamika BALI UNACHOFANYA NI KUNUNG'UNIKA TU. Na siku zote huwezi chukua hatua yoyote ile ukiwa unanung'unika.

 
Tutaendelea kulalamika mitandaoni bila kuchukua hatua hadi lini?

Mkuu tukichukua hatua say ya mass demonstration si unajua tena kazi ya mabomu ya kutoa utumbo njeee. Tanzania tumekuwa woga maana watu ambao wamekuwa werevu wamekosa voungo na wengine kuawa kabisa, tafakari matukio ya mabomu katika mikutano ya CDM na makanisa, waandishi wa habari makini kuumizwa au kuuawa kabisa. Watu kubambikizwa kesi kama tu wanapinga siasa chafu. Ila ninaamini watanzania wameamka na siku moja ushindi utapatikana.
 
kunahaja ya kukagua vyama hivi mara kwa mara na kuvifuta kabisa


Mifumo yetu iko very poor...Sheria ya uteuzi ilikuwa wazi kabisa kwamba kwa kila chama mjumbe mmoja atoke bar na mwingine Zanzibar. Sasa nini tena kilitokea...Yaani hapa hakukuwa na vetting yoyote jamani? Hii nchi hii...
 


Mkuu mimi sioni kosa la Dr Makaidi, manake alipeleka majina akijua akikosa yeye basi wife atakula shavu. Na sidhani kama alitegemea wote wapenye, hata yeye nadhani anashangaa.Pengine alijua wakifanya vetting basi watajua yule ni mkewe, lakini lahaula..Bwana mkubwa kapenda iwe hivyo....Majanga
 
Hakuna sababu ya msingi ya kuwaondoa; itabidi waondolewe na wengine wengi tu humo! Hakuna mahali sheria waliyoitunga wenyewe inakataza mtu na mkewe kutoka taasisi moja au nyingine kuwa wajumbe!
 
He just played a risk game to maximize his profit/opportunity, He deserved Congratulation

Kosa liko kwa aliye wachagua, hii inanipa picha kwamba hakuku kuwa na upembuzi yakinifi katika selection. Pia inanipa mashaka kwamba huenda wapo wengi sana humo ndani, Kaka, dada ashangazi mjomba baba mama jirani wawezeshaji na watu wa karibu.

Hili ni tatizo la kitaifa we need to be seriours even a bit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…