Mwananchi gani hataki Katiba Mpya? Tusisubiri ya Kenya

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628

Thursday August 19 2021

Na Daniel Mjema

Vuguvugu la madai ya Katiba mpya limeanza kushika kasi, lakini katikati ya vuguvugu hilo kumejitokeza kundi ambalo linajaribu kuuaminisha umma kuwa hakuna mwananchi wa kawaida anayeihitaji isipokuwa ni wanasiasa.

Kundi hilo limeamua kuvaa miwani myeusi katikati ya giza totoro na kwa vyovyote vile haliwezi kuona wala kukumbuka kuwa maoni pekee tuliyonayo hadi sasa ni ya wanaotaka Katiba mpya na aina ya Katiba na hatuna waliosema hawataki.

Tena maoni haya yalikusanywa chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba namba 8 ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya 2012 yaliyounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyokuwa na mamlaka ya kisheria kukusanya maoni nchi nzima.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni kwa miezi mitano kuanzia Julai hadi Desemba 2012 na ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi 1,365,337 ambao kati yao, 333,537 walitoa maoni yao.

Si hivyo tu, Januari 2013 Tume ilikusanya maoni kutoka makundi mbalimbali vikiwamo vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi na Asasi za kiraia na kwa ufupi makundi 160 yalikutana na Tume.

Ni kutokana na maoni hayo, ndipo tulipata rasimu ya pili ambayo ilipelekwa Bunge la Katiba na ikapatikana Katiba Inayopendekezwa ambayo kwa sehemu kubwa naweza kusema haikubeba maoni ya wananchi, bali maslahi ya wanasiasa.

Sasa wiki iliyopita nilipomsikia Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akisema hakuna mwananchi anayetaka katiba mpya nilishangaa sana nikajiuliza msingi wa kauli hiyo unajengwa kwa kuegemea utafiti upi?

Nikimnukuu Chongolo anasema “Wapi umeona wananchi wamebeba mabango wamesema wanataka katiba mpya. Tuambiane ukweli. Zaidi ya sisi wanasiasa. Na sisi wanasiasa katika katiba mpya tunataka mambo mawili matatu.

“Kwanza tunataka Tume Huru ya Uchaguzi, niambie mwananchi gani Tume huru inampelekea unga, inampelekea ugali. Tunataka tutengeneze loop hole (mwanya) wa sisi kushika madaraka. Full stop (mwisho). Hakuna kingine,” .

Lakini kiongozi huyo wa juu CCM hakuishia hapo, akasema kingine kikubwa wanachotaka (hao wanasiasa) ni demokrasia na uhuru wa kuendesha mambo yao na kwamba hayo ndio makubwa na akahoji “Niambie hii nchi haina uhuru?”

Ukifanyia tathmini kauli ya Chongolo na kurejea kilichojitokeza katika Bunge Maalumu la Katiba ambapo mambo ya msingi kabisa waliyoyataka yalinyofolewa, unajiuliza nani walikuwa wengi ndani ya Bunge lile zaidi ya wajumbe wa CCM?

Ukisoma ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya Mei 2018, imebainisha wazi kuwa mpasuko ndani ya Bunge la katiba ulichangiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wanasiasa ambao waliteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo.

Sasa kwa vile Chongolo anasema vuguvugu la sasa ni la wanasiasa wenye agenda zao za madaraka, basi tuachane na vuguvugu hili turudi kuanzia pale kwenye rasimu ya pili kwa sababu katiba inayopendekezwa ina maslahi ya wanasiasa.

Tuifumue sheria ya mabadiliko ya Katiba, tuwaondoe wanasiasa kuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, badala yake tutengeneze mfumo ambao rasimu ile ya pili itakwenda kupigiwa kura na wananchi ya Ndiyo au Hapana.

Ninasema hivyo kwa sababu tume ya Warioba haikulenga katiba ya vikundi au vyama vya siasa, bali iliandaa Katiba ya nchi ikiegemea maoni ya wananchi ambayo baadaye yalivurugwa katika Bunge Maalumu kwa maslahi ya wanasiasa.

Hakuna ubishi na ambaye halioni hili basi nitatilia shaka uzalendo wake, kuwa hoja ya Katiba mpya imeanza kuligawa taifa letu katika vipandevipande na kuibua chuki ambayo inaanza kutishia amani na umoja wa kitaifa.

Kuahirisha kuandika Katiba mpya ni sawa na kumpa panadol mgonjwa wa saratani ukiamini ni tiba.

Tusisubiri hadi vuguvugu hili la Katiba mpya likafikia kama wenzetu Kenya walipopitia wakapata Katiba mpya 2010 ambapo wapo walilopoteza maisha na wala hakuna sababu ya kutumia nguvu kuzima moto wa Katiba mpya.

Mwaka 1917 huko Urusi, Jeshi lililokuwa na vifaa vya kisasa lilizidiwa na nguvu ya umma na ndio maana nimetangulia kusema tusisubiri vuguvugu hili likaingia hatua nyingine kwa vile kulizuia itakuwa kama ni kuzuia mafuriko kwa mikono.

Chanzo: Mwananchi
 
CCM ya President SSH Ndio tu Hawataki Katiba Mpya , waliobaki Wanahitaji KATIBA hasa wale CCM wa tawala zilizotangulia wale wenzangu na mimi Mzoofu bin Taaban.
 
Kuna ule muungano wa vyama njaa eti navyo vinasema katiba mpya sio hitaji la watanzania kwa kwasasa
 
Cheyo, Chibuda, Lipumba, Hashimu na Yule wa ACT ..Hakuna Vyama Hapo ni Wasaka Tonge na Walamba Makombo ya CCM. Chama Cha Upinzani Tanzania ni Kimoja tu nacho ni CHADEMA.
 
Maccm yanaogopa sana Katiba Mpya, na Tume Huru ya uchaguzi! Yanajua fika kitakacho tokea baada ya hapo.
 
bado safari ni ndefu,wakati nyinyi wacahche mmafikiria kuhusu katiba,80%hawajui hata katiba inaathiri vipi maisha yao ya kila siku.

tunapowaambia muwe mnachagua agenda sahihi kwa wakati sahihi mnatuita MATAGA.
 
Thursday August 19 2021

Na Daniel Mjema.

Vuguvugu la madai ya Katiba mpya limeanza kushika kasi, lakini katikati ya vuguvugu hilo kumejitokeza kundi ambalo linajaribu kuuaminisha umma kuwa hakuna mwananchi wa kawaida anayeihitaji isipokuwa ni wanasiasa.

Kundi hilo limeamua kuvaa miwani myeusi katikati ya giza totoro na kwa vyovyote vile haliwezi kuona wala kukumbuka kuwa maoni pekee tuliyonayo hadi sasa ni ya wanaotaka Katiba mpya na aina ya Katiba na hatuna waliosema hawataki.

Tena maoni haya yalikusanywa chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba namba 8 ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya 2012 yaliyounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyokuwa na mamlaka ya kisheria kukusanya maoni nchi nzima.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni kwa miezi mitano kuanzia Julai hadi Desemba 2012 na ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi 1,365,337 ambao kati yao, 333,537 walitoa maoni yao.

Si hivyo tu, Januari 2013 Tume ilikusanya maoni kutoka makundi mbalimbali vikiwamo vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi na Asasi za kiraia na kwa ufupi makundi 160 yalikutana na Tume.

Ni kutokana na maoni hayo, ndipo tulipata rasimu ya pili ambayo ilipelekwa Bunge la Katiba na ikapatikana Katiba Inayopendekezwa ambayo kwa sehemu kubwa naweza kusema haikubeba maoni ya wananchi, bali maslahi ya wanasiasa.

Sasa wiki iliyopita nilipomsikia Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akisema hakuna mwananchi anayetaka katiba mpya nilishangaa sana nikajiuliza msingi wa kauli hiyo unajengwa kwa kuegemea utafiti upi?

Nikimnukuu Chongolo anasema “Wapi umeona wananchi wamebeba mabango wamesema wanataka katiba mpya. Tuambiane ukweli. Zaidi ya sisi wanasiasa. Na sisi wanasiasa katika katiba mpya tunataka mambo mawili matatu.

“Kwanza tunataka Tume Huru ya Uchaguzi, niambie mwananchi gani Tume huru inampelekea unga, inampelekea ugali. Tunataka tutengeneze loop hole (mwanya) wa sisi kushika madaraka. Full stop (mwisho). Hakuna kingine,” .

Lakini kiongozi huyo wa juu CCM hakuishia hapo, akasema kingine kikubwa wanachotaka (hao wanasiasa) ni demokrasia na uhuru wa kuendesha mambo yao na kwamba hayo ndio makubwa na akahoji “Niambie hii nchi haina uhuru?”

Ukifanyia tathmini kauli ya Chongolo na kurejea kilichojitokeza katika Bunge Maalumu la Katiba ambapo mambo ya msingi kabisa waliyoyataka yalinyofolewa, unajiuliza nani walikuwa wengi ndani ya Bunge lile zaidi ya wajumbe wa CCM?

Ukisoma ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya Mei 2018, imebainisha wazi kuwa mpasuko ndani ya Bunge la katiba ulichangiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wanasiasa ambao waliteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo.

Sasa kwa vile Chongolo anasema vuguvugu la sasa ni la wanasiasa wenye agenda zao za madaraka, basi tuachane na vuguvugu hili turudi kuanzia pale kwenye rasimu ya pili kwa sababu katiba inayopendekezwa ina maslahi ya wanasiasa.

Tuifumue sheria ya mabadiliko ya Katiba, tuwaondoe wanasiasa kuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, badala yake tutengeneze mfumo ambao rasimu ile ya pili itakwenda kupigiwa kura na wananchi ya Ndiyo au Hapan
Makala kutoka kwa mwandishi mchagga. Inaonekana wachagga ndio mnajua sana umuhimu wa katiba mpya 🤣🤣🤣
 
Watu makini hujadili message huwa hawajadili messenger.
 
CHADEMA mnataka katiba mpya yenye mfumo wa serikali 3 hakuna mwananchi mwenye akili timamu atakae hitaji katiba ya namna hiyo maana huo mzigo wa kuendesha serikali 3 utabebwa na wananchi

Na nyinyi CHEDEMA mnadai katiba mpya kwa tamaa zenu za madaraka mnajua katika hizo serikali 3 mnaweza mkapata japo serikali 1

Na ndio maana kila mkizungumzia katiba mpya mnazungumzia serikali 3 na tume huru ya uchaguzi kwa kuwa hapo ndio kunapatikana maslahi yenu

Hivyo nyinyi CHEDEMA hamdai katiba mpya kwa maslahi ya watanzania ila kwa maslahi ya matumbo yenu
 
Kuna shida mtu akitetea maslahi yake?
 
Lakini niwaulize ccm hivi kwanini hamtaki matokeo ya urais yapingwe mahakamani? Naomba mnijibu
 
CHADEMA mnataka katiba mpya yenye mfumo wa serikali 3 hakuna mwananchi mwenye akili timamu atakae hitaji katiba ya namna hiyo maana huo mzigo wa kuendesha serikali 3 utabebwa na wananchi

Na nyinyi CHEDEMA mnadai katiba mpya kwa tamaa zenu za madaraka mnajua katika hizo serikali 3 mnaweza mkapata japo serikali 1

Na ndio maana kila mkizungumzia katiba mpya mnazungumzia serikali 3 na tume huru ya uchaguzi kwa kuwa hapo ndio kunapatikana maslahi yenu

Hivyo nyinyi CHEDEMA hamdai katiba mpya kwa maslahi ya watanzania ila kwa maslahi ya matumbo yenu
Wakati wa mchakato wa katiba ya Warioba ulikuwa na umri gani.
 
Kama ccm inatetea maslahi yake ya kuendelea kubaki madarakani chadema wanakosea wapi na wao wakitetea maslahi yao ya kupata madaraka?
CHADEMA mnataka katiba mpya yenye mfumo wa serikali 3 hakuna mwananchi mwenye akili timamu atakae hitaji katiba ya namna hiyo maana huo mzigo wa kuendesha serikali 3 utabebwa na wananchi

Na nyinyi CHEDEMA mnadai katiba mpya kwa tamaa zenu za madaraka mnajua katika hizo serikali 3 mnaweza mkapata japo serikali 1

Na ndio maana kila mkizungumzia katiba mpya mnazungumzia serikali 3 na tume huru ya uchaguzi kwa kuwa hapo ndio kunapatikana maslahi yenu

Hivyo nyinyi CHEDEMA hamdai katiba mpya kwa maslahi ya watanzania ila kwa maslahi ya matumbo yenu
 
Cheyo, Chibuda, Lipumba, Hashimu na Yule wa ACT ..Hakuna Vyama Hapo ni Wasaka Tonge na Walamba Makombo ya CCM. Chama Cha Upinzani Tanzania ni Kimoja tu nacho ni CHADEMA.
Mnauliza Nani hataki katiba kwa sasa wakijitokeza mnawatukana eti walamba makombo Sasa hamtaki wasiotaka hiyo katiba waseme? Mnataka Kila mtu awe nyumbu kufuata matakwa ya gaidi wenu?
 
Wakati wa mchakato wa katiba ya Warioba ulikuwa na umri gani.
Warioba hakuandika katiba ila aliandika rasimu ya katiba

Ndani ya rasimu ya katiba kuna mambo mengi na ndio maana linaundwa bunge la katiba ili kuchuja yapi yanafaa yachukuliwe na yapi hayafai yaachwe

Kipengere cha serikali 3 hakina faida kwa wananchi kinatakiwa kitolewe kwa nini CHADEMA wanang'ang'ania kisitolewe

Huo mzigo wa kuendesha ikuru 3 mabunge 3 mabaraza ya mawaziri 3 mifumo ya mahakama 3 ataubeba nani kama sio wananchi

Narudia tena katiba mnayoidai hana faida kwa wananchi
 
Tusisubiri hadi vuguvugu hili la Katiba mpya likafikia kama wenzetu Kenya walipopitia wakapata Katiba mpya 2010 ambapo wapo walilopoteza maisha na wala hakuna sababu ya kutumia nguvu kuzima moto wa Katiba mpya.
Kenya hawajawahi pigania katiba mpya

Ilikuwa ni vita ya kikabila kati ya wakikuyu na jamii zao kwa upande mmoja na wajaluo na jamii zao kwa upande wa pili

WAkigombana kila mtu atawale kwake.Ndio wakaja na serikali ya majimbo ikabidi wabadili katiba ku accomodate serikali ya majimbo ambapo kila mmoja ni jogoo kwenye jimbo lake

Nchi zote walizotwangana kikabila au wao kwa wao YAANI Civil war huwa na seikali za majimbo

Mfano wa watu waliotwangana wao kwao barabara kwa vita za kikabila na kuanzisha serikali za majimbo kwa Africa ni nchi zifuatazo

1.Kenya
2.South Africa
3.Kongo
4.Nigeria
5.Sudan
6.Ghana

Kwa ulaya baadhi ni kama

1.Ubelgiji
2.Uingereza
3.Ujerumani

Kwa marekani

Ni Marekani Yenyewe ,Canada

ASia ni India ,Pakistan etc

Hizi zilikuwa forced na civil war zao kufikia katiba walizonazo vita zao hazikuwa za kutafuta katiba mpya noooooo

Kenya chanzo cha kuibuliwa katiba mpya haikuwa madai ya katiba mpya Civil war yao ndio ili force.Na kikwete ndie alienda kuwaamulia ngumi zao akawashauri haya ngumi hizo malizeni
 
Back
Top Bottom