Mr Brown Mzungu
Member
- Jun 10, 2020
- 11
- 15
Kampuni ya Mwananchi inayochapisha Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiaminika kwa kuhabarisha kwa uwazi iko kwenye msukosuko.
Pamoja na kushuka kwa biashara ya habari nchini, hali ya hewa so nzuri Mwananchi. Wafanyakazi wa idara ya matangazo wanasema kwamba kipindi cha mwaka mmoja, wamepunguza mamia ya wafanyakazi kwa takribani robo tatu, huku wakifikia hatua ya kutokulipa mishahara kwa wakati.
Hata ukiangalia habari zao zimekuwa ni kusifia, kujipendekeza ili waonewe huruma na serikali. Wafanyakazi wanasema tatizo ni uongozi wa Watanzania, kwani wakubwa wako kimaslahi zaidi na wanaishia kujigawia tenda za kampuni wapige pesa huku Waandishi wa Habari wakisota kwa mishahara kiduchu na wengine wakifanya kazi miaka zaidi ya kumi bila kupewa mkataba.
Waandishi wazuri wameondoka; hasa vijana kutokana na ubinafsi wa wahariri wao, ambao nao wameshajipandishia mishahara mpaka wafanyakazi wanaona hasira.
Wafanyakazi wanasema bora CEO Mkenya ama Tido Mhando waliisogeza kampuni kwenye mafanikio makubwa, lakini huu uongozi mpya uko busy na mambo yao binafsi na kampuni inadorora.
Hii inaonyesha kwamba, bila kujikomba, basi miaka mitatu ijayo hawatakuwa tena kwenye biashara.