Mwanandoa Kijana, usikubali Mwenza aue ndoto zako

Mwanandoa Kijana, usikubali Mwenza aue ndoto zako

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Vijana wengi mnakimbilia ndoa. Ni jambo jema, ila wengi wenu mkishaingia humo mnasahau malengo yenu katika maisha (career, business/ investment) maisha si kukopa benki na kununua IST/Crown baadae kujenga banda Mbagala au Mbondole bali fikiria investment hususani ya kuongeza kipato.

KAMWE Usikubali maneno ya shombo 'kukatisha tamaa' unapopambania ndoto yako.

Baba wa familia kuwa na picha pana ya maisha yenu ya baadae sio kushinda insta na ku-comment ukidhani umeyapatia

images (67).jpeg
 
Moja ya bandiko bora kabisa hili, mbaya zaidi unakuta kijana kasomeshwa kwa kuchangiwa changiwa na wazazi na ndugu, anapata kazi tu hata hajajipanga na kuwekeza vimiradi vidogo vidogo ambavyo angeweza kutoa hata viajira kwa ndugu zake au wadogo zake njemba inawahi kuoa halafu mwanamke anaitawala inasahau ilikotoka.
 
Vijana wengi mnakimbilia ndoa. Ni jambo jema, ila wengi wenu mkishaingia humo mnasahau malengo yenu katika maisha (career, business/ investment) maisha si kukopa benki na kununua IST/Crown baadae kujenga banda Mbagala au Mbondole bali fikiria investment hususani ya kuongeza kipato.

KAMWE Usikubali maneno ya shombo 'kukatisha tamaa' unapopambania ndoto yako.

Baba wa familia kuwa na picha pana ya maisha yenu ya baadae sio kushinda insta na ku-comment ukidhani umeyapatia

Very true. Kuna jamaa alioa akiwa masomoni huko ng'ambo (Leeds University) ile baada ya honeymoon songombingo likaanza mwanamke anataka pesa tu jamaa hela ya scholarship ndo alitegemea aishi kule ughaibuni mke haelew, mpaka December 2020 jamaa alikua hajamaliza PhD Yake toka 2013. Kazini kafukuzwa na masomo hajamaliza
 
fikiria investment hususani ya kuongeza
Mkuu kwa mazingira ya Tanzania utawalaumu bure vijana. Mazingira ya uwekezaji siyo stable.

Nikupe mfano mmoja tu. Kuna watu walikopa benk wakawekeza kwenye kilimo huko Katavi akiwemo Sumry aliyeuza mabasi yake 80 na kuingia kwenye kilimo.

Baada ya kuvuna akatokea mkuu wa wilaya na kupiga marufuku kuuza mahindi nje ya wilaya yake. Hii ni kufuatia marufuku ya iliyotolewa na rais Magufuli mwaka 2017.

Hata Sasa unavyoona malori ya mahindi pale mpakani mwa Kenya ni fedha za watu zinapotea.
 
Very true. Kuna jamaa alioa akiwa masomoni huko ng'ambo (Leeds University) ile baada ya honeymoon songombingo likaanza mwanamke anataka pesa tu jamaa hela ya scholarship ndo alitegemea aishi kule ughaibuni mke haelew, mpaka December 2020 jamaa alikua hajamaliza PhD Yake toka 2013
sipati picha jinsi alivvyo sasa
 
Back
Top Bottom