Kuwa na marafiki wa jinsia yoyote si kosa, tatizo ni kuwa katika utamaduni wetu wengi tunaona kama hilo haliwezekani. Wengi tunaamini kuwa haiwezekani kuwa na urafiki na jinsia nyengine bila matamanio.
Tatizo kubwa zaidi ni pale wewe na mwenzako mnapokubaliana (au kuvumiliana) kuwa na marafiki wa jinsia tafauti, lakini bado wanajamii wataliona hilo ni kosa na wataanza kuwatia fitina.
Lakini ukuwachia jamii inafikirije, jiulize wewe mwenyewe kwanza, "utakubali mwenza wako kuwa na (ma)rafiki wa jinsia tafauti? Isiwe ni "one way right", i.e. mwanamume anaweza kuwa na rafiki wa kike lakini mwanamke asiwe na rafiki wa kiume.