kwanza nampa Pole sana!
Kuna maswali itabid Anisaidie..
- Kwenye Ukoo au familia kuna watu/Mtu ana kigugumizi au ndugu yake yoyote ana kigugumizi?
- Mtoto alichukua Muda gani kulia kipindi anajifungua vipi anaweza kujua APGAR score ya Mtoto?
- Amewahi kuanguka kudondoka kwa kuangukia Kichwa? au kupata ajali yoyote?
- Watu wanaomzunguka au Kumlea (Dada wa kazi na wengine) hawana Kigugumizi??
Hata hivyo nimtoe hofu tu kwamba kwenye kipindi cha Speech development hasa mtoto akiwa Na miwaka 1 na nusu mpaka miaka mitatu..
hupitia mabadiliko mengi sana na huweza kuaddapt mazingira anayokutana nayo hasa kwenye upande wa Maongezi haraka sana Hivyo anapaswa kuwa makini na kumuongelesha mtoto mara kwa mara ili aweze kutengeneza Lugha kwenye akili na ubongo wake..
Pia kumbadilishia Mazingira mtoto Kwenye kipindi hicho pia sio vizuri sana namaanisha kuhama hama sehemu..Inamfanya ashindwe kuzoea mazingira..
Hata hivyo linaweza pia kuwa Swala la Neurological speech Development na atahitaji Vipimo zaidi,
Na huenda Akawa na Underlying Medical Condition kama Autism au Cerebral palsy so nashauri angempeleka Hospitali Kwa uchunguzi zaidi..
CC:
runyaga