DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Haya yule Dokta Uchwara mwenye D MBILI anayejiita marisi schwein aje humu aone mabosi zake walivyochukua hatua madhubuti za kuwakamata wahusika.

Kimbelembele kinaponza. Hasa ukiwa na D MBILI.

Daktari gani una D MBILI? Hii TCU inatuletea majanga katika Taifa.
 
Uzuri ni kuwa, hakukuwa na mazungumzo kati yangu na yy kama ilivyoandikwa hapo juu. Sijui haya katunga nani
Mheshimiwa don't use that words, inasikitiaha sana kuuliwa kwa binadamu kizembe hata kama hukuzungumza ila tukio limetokea na maisha yametoweshwa.

Hapo ni mtu/watu wawajibishwe no excuse tupo kwenye Ramadhan tutende haki hata kwa wasio na uwezo kujisimamia, waweze kusimama.
 
Si ndiyo taarifa imetolewa kuhusu maendeleo ya shauri ndugu yangu? Mm nilichokanusha ni kuwa sijaongea kwa simu na kutoa hayo maelekezo kama ilivyosemwa. Kisha nikatoa na update ya hatua zilizochukuliwam kumbe tena ndugu yangu sijafanya vema? Niwie radhi basi tusonge mbele.
 
Achana nae
 
Inaumiza sana kwa kweli,mara nyingi mauaji ya visasi huanzia katika Hali Kama hizo hususan haki inapopindishwa na ndugu wakabaki na majeraha ya moyo.

Huyu mama asaidiwe
 
Nakupenda Waziri wangu, miongoni mwa wachache walio tayari kujibu hoja za watu wa hali zote. Be blessed.
 
Umemchapa mtoto, kafa lazima ujieleze kilichotokea sio unafichwa fichwa kama mwali. Kama ulimchapa kwa weledi kwanini unafichwa fichwa? Unatetea ujinga ujinga tu.
Usipende kusikiliza upande mmoja na kujaji? Kwa Hiyo unataka kusema Mwl kampa Hela Daktari atoe ripoti feki, akampa waziri na mtu wa Dawati la jinsia wafiche ukweli? Hivi unadhan ni rahisi? Hivi unaijua case ya mauaji? Unajua namna serikali inamvalue mwanafunzi? Mwaka Jana nilipatwa na mkasa mmoja. Nilimuokota mwanafunz mmoja njiani akiwa amelala anatetemeka. Kwa maelezo yake, mwenzake amemchoma na pen kichwani baada ya ugomvi Watu wametawanyika ndio yeye hali ikabadilika. Kiutaratibu ilitakiwa nianzie police kupata form ya pf3 ila nikamuomba Daktari amsaidie tu maana anahitaji matibabu ya haraka. Bahati mbaya mtoto akafariki kesho yake. Nikashangaa police wananing'ang'ania Hata maelezo yangu hawayasikilizi. Badaye nikaona mkuu wa kituo anataka kuonekana ameshaanza kuchukua hatua na baadhi ya watu tayari wapo ndani. Nikamuomba mkuu wa kituo anisaidie kutoa pf3 na kuibackdate akasema haiwezekani Maana taarifa za Jana za kituo ameshatuma mbele na haiwepo hiyo taarifa. Hospital pia hawawezi kubadili taarifa maana pale wanajiendesha kidigitali taarifa zote zinatembea Kwa njia ya Mfumo wa computer. Niliteseka sana kuja kutoka. Na ilikua ni baada ya kumkamata mtoto aliyemchoma mwenzake na pen. Ninachotaka kukwambia hapa ogopa case ya kumuua mwanafunzi, mambo sio marahisi Kama mnavyodhani mtaani. Maana Daktari mkuu hataki kuharibu Kazi yake, police pia ni hivyo hivyo, Kila mtu anajiweka safe side. Maana case inaweza kufika Mbali na udanganyifu wowote unaweza kumkost mtu

turudi kwenye Mada Mimi nadhani ripoti ya Daktari ni ya Kweli, lakini mzazi hataki kuamini Hilo, anapeleka malalamiko Kwa waziri akiwa tayari na majibu yake, anataka Watu waadhibiwe tu Ili Moyo wake uridhike. Kilichotokea hapo ni matukio mawili yasiyo na mahusiano yametokea, mwalimu kuadhibu na mtoto kuonyesha dalili za cancer na Hilo ndio mzazi hataki kuamini hilo.

Inauma sana kumpoteza mtoto lakini inahitajika utulivu tu, ni Kweli mzazi anaham ya kumpigania mtoto angalau Mwl achukuliwe hatua Ili mtoto huko alipo ajue mzazi hakukaa kizembe kudai haki. Ila Ndugu mzazi jikaze, limeshatokea na haiwezekani kubadili Hilo na maisha lazima yaendelee
 
Habari bado haija balance .....ni mbaya sana kuleta habari upande mmoja....inaharibu maana
 
Unadhan mpaka waziri na mtu wa Dawati la jinsia kuanza kumpuuza mzazi hawakulifanyia Kazi Hilo? Lazima Mwl amehojiwa na Daktari amehojiwa. Lazima mkurugenzi amelifatilia analijua Hilo, lazima mkuu wa wilaya amelifatilia analijua Hilo, DSEO Lazma amelifatilia analijua Hilo, ocd lazma analijua hilo Maana waziri hawezi kwenda mwenyewe Ana vyanzo vyake vya habari na viongozi wa chini hujitahid sana kufatilia jambo na kulifahamu Kwa kina, asije kupigiwa Simu akampotosha waziri Au akajibu hajui Maana ni kuchezea kitumbua chake.
 
Dada pole sana
Yaweza kuwa fimbo zimekuw sababu ya kusogeza kfo chake karbu , lakn sasa mwanafunz/Mtoto (07) ata kama huyo.mwl ni wa field kweli amempga ngumu

Kwa maelekezo ya awali inaonyesha fimbo lakn inaonyesha changamoto ilipozd mkaja tafuta sababu zaid mkadai ni ngumi pia

Kawaid ulipofk hospital ya kwanza kuna report inaandikwa vle mgonjwa hali yake ilivyo iliandw kuhusu majeraha ya fimbo

(Pia tafuta wanafunz wanao soma na mwanao uliza ni kwa jins gan mtoto alipewa adhabu)
 
Don't jump to conclusions
 
Pole sana bi dada .siku za mja zikishatimia huwa sababu ni nyingi sana
Mtoto ndio ameshafariki mshukuru tu mungu
 
DED alifuatwa kuulizwa na mwandishi wa habari anajibu simple tu. " mtoto amekufa kwasababu ya cancer" pumbafu kabisa yaani hii nchi Ina viongozi wa ovyo mpaka unashangaa Huwa wanateuliwa kwa vigezo Gani?
Ajajibu simple hiyo kesi itabebwa na ushahid wa namna mbili
1:- ushahid wa kitabibu (ushahid mkuu) ndio TD ameuzngatia

2:- Ushahid wa mazingr kutok kwa wanafunzi


Ushahid na 1 ni muhimu kuhusian na ushahid na mbili,

Hospital:- mtoto alifikishwa akiwa na majerah makubwa (@alishambuliwa na kuumizw sehemu fulan ambako kulipelekea hali yake kuzorota na kufa

Wanafunz:- mwalimu alimchapa na kumpga ngumi ....
 
Mheshimiwa Waziri kwanza nikupongeze kwa kujibu haya maswali, ila si jambo sahihi kuanza kutoa lawama kwa huyo mama elewa yupo katika kipindi kigumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…