Mwanangu ana joto lisilokoma, hasa nyakati za usiku

gashambala uwezo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
485
Reaction score
67
Habari ndugu zangu,

Mwanangu tangu tarehe 9/2 alikuwa anaharisha, tukampeleka maabara kapimwa kinyesi (stool), tuliomba apimwe kipimo kimoja tu, na kukaonekana kuna Amiba, dakitari alituandikia dawa za kununua (metronidazole benzoate suspension).

Dawa hii hatukununua mana'ke tulikuwa nayo, hiyo tulienda nyumbani na kuanza kumpa dawa .

Hata hivyo usiku alishikwa na joto la khali ya juu sana lililo ambatana na kushituka shituka, kesho yake tena tukaenda kumpima malaria, ambapo alionekana hana malaria, jioni hali ilizidi, tukaamua kununua tu dawa ya Malaria tukiamini kwamba pengine ile dawa ya kwanza ilifanya wasiione malaria (tulinunua mseto ya watoto).

Hata hivyo, siku ya Ijumaa hali yake haikuwa nzuri, tukaamua kumpeleka njilani kuna kadispensary, tukamwelezea na akamwandikia dawa hizi, mwanzo alionekana amepona lakini hali imerudi tena. Aliandikiwa dawa hizi; (Alatrol syrup na toto-mal. Paracetamol suspension)

Msaada!
 
Mpeleke mtoto hospitali acha kujitia ubahili na ujuaji wa kujinunulisha dawa!!!!

Siulizi lolote sababu mtoto anatakiwa kwenda hospitali tu
 
gashambala uwezo

Mwanao anaumwa hujui anaumwa nini unampeleka hospitali unaamua kumpima kipimo unachotaka wewe kama vile unajua tatizo. Haya tatizo limeonekana unaandikiwa dawa unagoma kununua unaenda kumpa dawa uliyohifadhi kwenye mazingira unayojua wewe!

Hivi huogopi kucheza na uhai wa mwanao? Rudi kwa Daktari wako wa kwanza umpime kila kitu na umweleze ile dawa aliyokuandikia hukununua ila umempa dawa uliyoihifadhi kwenye kabati nyumbani kwako!
 
Last edited by a moderator:
wewe unahitaji makofi mtoto anaumwa unaleta mjadala JF, mpeleke kwa daktari wa watoto acha ubahili
 
Mijitu mingine sijui imerogwa? Yaani badala yakufuata alichokueleza dr, unatafuta ushari humu, pumbavu kabisa
 
Alikuwa anaharisha, ana homa na "kushitukashituka" hizi dalili zote sio nzuri kiasi cha kuanza mjadala mtandaoni

Ni kweli Kabisa nakubaliana na wewe mkuu na nilimuuliza mtoto ana umri gani ili kitu cha kwanza nimueleze possibilities na pia ampeleke mtoto hospitali.
 
Ni kweli Kabisa nakubaliana na wewe mkuu na nilimuuliza mtoto ana umri gani ili kitu cha kwanza nimueleze possibilities na pia ampeleke mtoto hospitali.

Ok mkuu. Ukimuona mzabe makofi kwa niaba yangu dhambi ntabeba mie
 
gashambala kama upo dsm mpeleke kinondoni b pana dktr mzur wa watoto hata hivyo

siku ya pili haikutakiwa mlale hadi asubuhi ilipaswa kwenda hosp isiku. dkt atajua ampe nini...nb awe dkte wa watoto tafadhali.

pili, UTI inadalili hizo
 
ok!, nyote nawashukuru sana kwa mawazo yenu, hata hivyo si dhani kama kweli nasitahili makofi tulipima hatukununua dawa kienyeji. Asante
 

mkuu umenigusa sana na maelezo yako, watu wengine sijui wanafikiria nini, dawa umeifungua labda imekaa zaidi ya wiki mbili ndani unaenda kumpa mtoto, halafu anaamua tu kumpa dawa mseto na vipimo vinaonesha hana malaria duh hii ni zaidi ya kutokujali afya ya mtoto
 
nenda kwa wamasai wana dawa ya huo ugonjwa inaweza kuwa ni degedege.
 
ok!, nyote nawashukuru sana kwa mawazo yenu, hata hivyo si dhani kama kweli nasitahili makofi tulipima hatukununua dawa kienyeji. Asante

Pole kaka kwa makofi, ila afya ya mtoto ni suala sensitive sana hapo ulifanya makosa.
Mungu akuongoze kuwa baba bora!!!!

Mrejesho wa afya ya mtoto ni vipi??!!!
 
nenda kwa wamasai wana dawa ya huo ugonjwa inaweza kuwa ni degedege.

Acha hiyo maneno "convulsion" haina dawa kwa wamaasai, dawa ni kuondoa chanzo cha homa na huyo degedege anahama jumla!!!!

Ambia na wenzio maneno hii. . . . . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…