Mwanangu anaweza pata shule ya advance kwa matokeo haya


good!umejibu kitaalam sn,wengine wote wamekurupuka tu kujib wasiyoyajua!
 
Div 4 ya 26
BIO C
CHEM C
PHY D
GEO D
KISW D
HIST D
CIV D
ISLAMIC D
MATH F
YEYE ANAPENDA ASOME PCB AU CBG nisaidieni shule ambayo itamchikua huyu mwanangu

Hizi ni combination za Sayansi ambazo masharti yake lazima kufaulu hisabati. Kwa kuwa hajafaulu hisabati itakuwa ngumu kuchaguliwa shule ya Serikali. Ila private anaweza kuingia kwa masharti ya kurudia mtihani wa hisabati. Angefaulu hisabati, hata kwa D angekuwa na C,C, D sasa hivi ungekuwa unachekelea. Kwa matokeo hayo wasikudanganye bure, mtoto hana credit za kutosha huyo.
 
kama shule gani

Kwa matokeo yalivyo mabovu kiujumla hata shule za serikali atapata!ila inategemea kama yeye anataka private au government


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Huyo kijana hawez kusoma fom5 sio govt tu bali hata private unless mwaka huu kuwe na mabadiliko ktk vigezo vya kujiunga na fom5!

Kimsingi ili mwanafunzi aweze kusoma A'level ni LAZIMA awe amepata credits zisizopungua 3!!bila kua nazo hatoruhusiwa kufanya mtihani wa fom6!!

Je mwaka huu serikali imetangaza mabadiliko ya masharti ya kujiunga na A'level??km hawajabadilisha masharti basi nyie mlomwambia kua anaweza kusoma A'level mmetoa wapi ujasiri huo?
 
Mm nakusha mpelekw chuo aanze certificate then diploma mpk degree, kuresit ni kazi sana maana Ana crdt 2 angekuwa na 3 angepata shule,
 
Mm nakusha mpelekw chuo aanze certificate then diploma mpk degree, kuresit ni kazi sana maana Ana crdt 2 angekuwa na 3 angepata shule,

mtoto habari na chuo now hana kabisa ye anataka kupitia advance
 
Akiweza ajaze fomu ya wizara ya Afya kama ana interest ya kuwa daktar baadae.asome diploma ya Clinical medicine.au hata certificate ambayo ni miaka miwili baadae atasoma diploma mwaka mmoja.KWA ADVANCE MPAKA AWE NA CREDIT TATU
 
Akiweza ajaze fomu ya wizara ya Afya kama ana interest ya kuwa daktar baadae.asome diploma ya Clinical medicine.au hata certificate ambayo ni miaka miwili baadae atasoma diploma mwaka mmoja.KWA ADVANCE MPAKA AWE NA CREDIT TATU
yaani anavyoitaka advance mkuu
 
Nampa pole no way out.Akubaliane na uhalisia wa matokeo.La sivyo itabidi arisiti mpaka aipate hiyo credit moja.Akichelewa anaweza kupoteza mwaka bure.Awe na akili ya kiutu uzima sasa.ASIWE MBISHI KTK OPTION AMBAZO WATU WANAMPA KAMA MAWAZO ZITAMSAIDIA
 
Nampa pole no way out.Akubaliane na uhalisia wa matokeo.La sivyo itabidi arisiti mpaka aipate hiyo credit moja.Akichelewa anaweza kupoteza mwaka bure.Awe na akili ya kiutu uzima sasa.ASIWE MBISHI KTK OPTION AMBAZO WATU WANAMPA KAMA MAWAZO ZITAMSAIDIA
asante mkuu kwa mchango wako wa mawazo
 
nimeambiwa now hata credit mbili za komb ya science unasoma bila kutafuta c nyingine,

Aliyekwambia hana taarifa sahihi. Hauwezi kusoma A'level bila kuwa na credit kuanzia 3. Hapo inabidi arudie baadhi ya masomi huku akiendelea kusoma A'level. Ningemshauri asome CBG kama anapenda sayansi, kwa PCB, Physics itamsumbua manake anaonekana hayupo vizuri kwenye hesabu.
 
Af kingine kama unauwezo wa kumsomesha chuo mpeleke akasome certificate, hizi biashara za kurisiti au kosoma A'level siku hizi naona sio kabisa anaweza akarisiti mara mbili na credit asipate na hapo anakuwa amepoteza muda. Na anaweza akapata na akaenda A'level af matokeo yakawa sio mazuri tena. Bora aanze kuwa na professional mapema kwa kusoma certificate. Ninavyoamini mimi elimu ya secondary ni ngumu mno kuliko ya chuo.
 
Jaman, acheni kudanganyana hapa..hamna shule yoyote inayopokea fom 5 mwenye chn ya crdt 3..mbona mnataka kumchafua braza wangu wa majengo..fom fv wt 2 credt dat z day drm..labda kama kuna mabadiliko yamefanyika ucku
 

ahsante mkuu kwa mchango wako
 
Kusoma fom 5 serikali wt dv 4 hyo ktu haipo...labda kama sera ya elimu imebadilishwa n cjui hayo mabadiliko yalifanywa ln
 
sawa mkuu ila mkuu mwenyewe anadai alikuwa vizuri sana kwenye GEOGRAPH na KISWAHILI anadai nimpe fedha aka appeal hiyo mitihani miwili je mkuu vp kuhusu matokeo ya kuappeal
 
Div 4 ya 26
BIO C
CHEM C
PHY D
GEO D
KISW D
HIST D
CIV D
ISLAMIC D
MATH F
YEYE ANAPENDA ASOME PCB AU CBG nisaidieni shule ambayo itamchikua huyu mwanangu

Shule ya private yoyote watamchukua ila form 6 hatoruhusiwa kufanya pepa kutokana na hana credit 3 yaani c 3 na kuendelea.
Iliyopo asome six huku anarisit ama kama unajiweza kifedha aende chuo kwa kuanzia certificate 1year then diploma 2years na kuendelea digree 3years. Ila kurisiti credit zinapatikana kwa taabu kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…