UWOGA=UMASKINI
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 2,399
- 1,014
pole sana mkuu mara nyingi watoto wanaotambaa kwa kusota wanachelewa sana kusimama hasa inawakuta watoto wa kiume. Endelea kumfanyisha mazoezi ya kutambaa ikiwezekana mnunulie kigari kile cha mbao ili atamani kukishika na itapelekea atamani kukisimamia, usichoke mkuu hata wa kwangu alikuwa hivyo
nimemtengenezea hakitaki hata kukigusa je wewe ulifanyaje bro na wako alitembea au kuongea na umri gani
Pole sana mkuu..mimi kama mzazi pia ninasikia uchungu
kwa ulichokieleza hapo juu...cha kukushauri wewe
muendelezee mazoezi ya kutembea kama hana matatizo
ya kilema cha kutembea basi amini kuna siku atasimama
na kutembea tu...
kwani kuna hata watoto wengine waliisha chelewa kuongea
mpaka mzazi anadhani labda mtoto atakuja kuwa bubu ila
mwisho wa siku mtoto anakuja kuongea...na kisha wanaanza
kubonga kwa sana tu.
wadau wa hapa nisaidieni cha kufanya mwanangu ana mwaka na miezi saba lakini hawezi zungumza au kutembea na anatambaa na matako yaani anasota na nimemmpeleka kwenye mazoezi toka mwaka jana na kwa maombi sana.kama kuna mtaalama ana kitu kingine aniongezee ili huyu kijnana wangu wa kiume afanye yale yampasayo kufanya na umri alio nao...