"Mwanangu huna nidhamu" dedication diss song to producer Master Jay " MJ records" by Dudu Baya

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
MSANII DUDU BAYA.


Msanii Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu baya, amefunguka juu ya wimbo ambao ulimpa umaarufu " Mwanangu Huna nidhamu"

Msanii Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu baya, amefunguka juu ya wimbo ambao ulimpa umaarufu wa mwanangu huna nidhamu, na kusema wimbo huo lilikuwa dongo la Master Jay.

Dudu baya alisema aliuandika wimbo huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha Master Jay kumtupia pesa yake aliyompa ya kurekodi, baada ya kumjia juu kwa nini hawajerekodi kwa muda kama walivyokubaliana.

“Unajua kipindi hiko mi nilikuwa nakaa Tegeta, na Master jay alikuwa anakaa kwa baba yake, sasa kila Jumamosi ndio alisema njoo urekodi, kipindi hiko na kina Mr. II (Sugu), sasa siku nyingine unakuta dingi kashampa kazi nyingine anafanya, so anakuwa hana muda, siku moja nikamwambia vipi unazingua ujue! Akatutupia hela zetu chini, si ndo tukaenda tukarekodi kwa Minje na ngoma ikawa hiti”, alisema Dudu baya.

Pamoja na hayo Dudu baya amesema ila Master Jay ndio alikuwa producer wake wa kwanza kumpa hela, na alimpa shilingi elfu kumi ambayo kwa kipindi hiko ilikuwa kubwa.

Akiongelea kuhusu msanii ambaye alikuwa chini yake Dogo Hamidu kwa sasa 'Nyandu Toz, Dudu baya amesema anajivunia mafanikio ya msanii huyo, kwani kwake ni kama mtoto wake kwani mama yake alipofariki alimwacha mikononi mwake.

“Unajua hata mama yake Nyandu alivyofariki aliniambia nakuachia mwanangu, nilelee mtoto wangu, na Nyandu hakuwahi kumjua baba yake, so nikawa namlea Nyandu kama mwanangu, nikamwambia dogo sikupeleki studio mpaka usome kwanza. Ndio akaenda shule, ila kwa sasa najivunia mafanikio yake kwani ni sawa na mtoto wangu mwenyewe”, alisema Dudu Baya.

Kuhusu kipigo alichowahi kumpa Nyandu Toz baada ya kuacha chenji ya sh. 300 dukani, Dudu baya alisema alimpiga ili kumfundisha juu ya matumizi ya hela, na si vinginevyo ..

https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/100064569174258/posts/pfbid0j9L8CAS7ZEoAao5sfs9WtpjUXKVQgQfvSQHXGafsQAs8aJwYHPFvHoTU3XJX5BkVl/?app=fblUkwaju wa kitambo
0767 542 202..



 
Mbona insemekana huo wimbo alitunga kumchana live mshikaji Fulani wakuitwa Rashidi (chidi) aliyekuwa ni kunyozi pande za hapa tegeta. Insemekana chidi aliwahi baba yake mzazi kwamba "ww siyo baba yangu, sikutambui na usinifuate fuate"

Kipindi hicho wapo maskani moja baaab kubwa hapa TEGETA. WEST COAST HAIR CUTTING SALOON. Matozi wote wa tegeta Hilo ndilo camp lao,

Baada ya tukio la chidi kumtukana baba yake, ndipo double G akatoka na ngoma, MWANANGU HUNA NIDHAMU.

PIA insemekana ule wimbo wa dege la jeshi, aliimba baada ya kukataliwa kimapenzi na dada mmoja wakuitwa......... Dudu akatoa huo wimbo kumshambulia na kumharibia huyo dada.
 
Hahahahahaha!
Nyandu kachezea mkong'oto kisa kasahau 300/= dukani.
Hi ii inafurahisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…